Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ninja ni Yanga tu

Muktasari:

HUU mfumo wa uchezaji wa Yanga hasa inapocheza na Simba SC huwa ni kujilinda zaidi na kufanya mashambulizi machache ya kushtukiza hivyo lazima Wekundu wa Msimbazi wafanye sana kazi ili washinde mechi zao.

Marlow kichwa kingine

YAANI huyu Marlaw ni bonge la msanii ila sijui imekuwaje. Tatizo la Watanzania ni U-Ali Kiba na U-Diamond ndiyo unapelekea hata huyu jamaa asisikike au asiongelewe kabisa ila kwa wanaomjua Marlaw kazi zake si mchezo na zinakubalika kama ninavyozikubali mimi.

Rashid Ramadhan

Ninja ni Yanga tu

ABDALLAH Shaibu ‘Ninja’ anastahili kucheza Yanga tu lakini si kwa Simba maana staili yake ya kucheza haifanani na kimataifa kabisa bali Yanga. Anabutua butua tu mipira, alipigwa chenga moja hatari sana na Zana Coulibaly mpaka akakaa, alishindwa kuzuia krosi ya kuchopu ya nahodha wa Simba, John Bocco.

Rashid Kitiku

Yanga noma

HAKUNA kuogopa Yanga ni Yanga tu, tupo pamoja wadau kazi ni moja tu kuhakikisha tunazidi kushinda.

Saddam Lubida

Kama tulikuwa wote

MWANDISHI aliyemkumbuka Marlow namshukuru sana kwa kuniulizia maswali haya ambayo hata mimi nimekuwa najiuliza mara nyingi yaani ni kama ulikuwa na mimi. Kwa hili hapa nafikiri tutapata majibu sahihi kuhusu Marlow.

Zacharia Lughano

Beki hasifiwi

Beki Abdallah Shaibu ni jembe haswa. Hayo mambo ya fujo nani kakwambia beki anasifiwa, huwa hasifiwi. Hongera kwake Ninja jamaa kama Sergio Ramos kwani ukienda kizembe anakufyatua tu.

Fred Clement

Yondani umezingua

KITENDO cha Ibrahim Ajibu kuwashika mikono wachezaji wenzake kweli si sawa lakini pia isingekuwa jambo la jinai kama Kelvin Yondani ‘Vidic’ angempa mkono mwenzake.

Ikupilika Sakuka

Kuifunga Yanga kazi

HUU mfumo wa uchezaji wa Yanga hasa inapocheza na Simba SC huwa ni kujilinda zaidi na kufanya mashambulizi machache ya kushtukiza hivyo lazima Wekundu wa Msimbazi wafanye sana kazi ili washinde mechi zao.

Rashid Kitiku

Zahera profesheno

KOCHA wa Yanga Mwinyi Zahera ameonyesha kuwa ni profesheno kwenye soka baada ya kukubali kuwa Simba iliwazidi kiwango, safi sana. Hii si kama hawa rafiki zangu wengine wanaojifanya mashabiki kindakindaki kelele tupu.

Jumaa Farijallar

Mkongo si mnafiki

HIVI kwa nini Mwinyi Zahera asiukubali mziki wa Simba kwa sababu Kwann huyu kocha si mnafiki anasema ukweli ingawa wakati mwingine kauli zake hizo za kusema ukweli zinaweza kumweka matatani.

Must Swaleh Kongowea