Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ngoma ayatolea macho makombe matatu Simba

Muktasari:

  • Ngoma ndiye aliyefunga bao pekee kwenye ushindi wa 1-0 walioupata Simba dhidi ya JKT Tanzania, jana Jumatatu kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Dar.

BAADA ya kuipa pointi tatu Simba kwenye mchezo dhidi ya JKT Tanzania, kiungo Fabrice Ngoma amesema ubora anaouonesha ni kuhakisha timu hiyo inatwaa mataji yote matatu wanayoshiriki.

Ngoma ndiye aliyefunga bao pekee kwenye ushindi wa 1-0 walioupata Simba dhidi ya JKT Tanzania, jana Jumatatu kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Dar.

Akizungumza na Mwanaspoti, Ngoma amesema kutokana na matokeo wanayoyapata licha ya ugumu wa ratiba, ana imami kubwa ya wao kuendelea kufanya vizuri mechi zote zilizobaki na hatimaye kutwaa mataji wanayowania ambayo ni Ligi Kuu Bara, Kombe la Shirikisho Afrika na Kombe la FA.

“Hakuna mchezo rahisi, kwetu yote ni migumu ukizingatia ratiba tuliyonayo tunacheza mechi kila baada ya siku mbili, sio rahisi lakini sisi kama wachezaji malengo ni kufanya vizuri kwenye kila mchezo na hatimaye kutwaa mataji,” amesema na kuongeza.

“Mchezo wetu na JKT Tanzania ulikuwa mgumu, haukuwa rahisi, tumepambana na hatimaye kufanikiwa kukusanya pointi tatu, sasa tunautazama mchezo mwingine ulio mbele yetu lengo ni lilelile kukusanya pointi tatu.”

Kiungo huyo mwenye mabao manne kwenye Ligi Kuu Bara, amegusia mkataba wake ndani ya timu hiyo ambao unamalizika mwisho wa msimu huu.

“Kwa upande wangu mimi kama mchezaji kazi yangu ni kucheza mpira, ndicho ninachokifanya, kuhusu mkataba wangu unaenda kumalizika, hivyo nasubiri uongozi wa Simba utafanya uamuzi gani juu yangu,” amsema Ngoma.