Ngoma atua Taifa aishudia Azam

Muktasari:

  • Mzimbabwe huyo amejiunga na Azam akitokea Yanga msimu huu

Dar es Salaam. Mshambuliaji mpya wa Azam, Donald Ngoma ameibuka uwanjani kuangalia mechi fainali ya Kombe la Kagame kati ya timu yake mpya dhidi ya Simba kwenye Uwanja Taifa, Dar es Salaam.

Hii ni mara ya kwanza kwa Ngoma kuonekana nchini tangu aondoke kwenda Afrika Kusini kwaajili ya matibabu.

Ngoma alifika uwanjani hapo na kupokelewa na mchezaji mwenzake Tafadzwa Kutinyu na kisha walikaa pamoja.

Katika dakika 45 za kipindi cha kwanza muda wote alionekana kuangalia mpira kwa umakini na kuelekezana baadhi ya vitu na mwenzake huku wakiangalia zaidi upande wa ushambuliaji.