New City yashuka rasmi, Mlandege yapaa nafasi ya pili ZPL

Muktasari:
- Wakati New City ikipokea kilio cha kushuka daraja rasmi baada ya kupoteza mchezo jioni ya leo kwa kupigwa mabao 5-1 kutoka timu ya Mwenge, Mlandege imepokea kicheko cha kuifunga Uhamiaji mabao 3-1 na kupanda nafasi kutoka nne hadi ya pili na kufikisha pointi 53.
TIMU ya New City imeshuka daraja rasmi baada ya jana kupoteza kwa kupigwa mabao 5-1 na Mwenge ambayo nayo inapambana kuepuka kushuka daraja kutoka Ligi Kuu ya Zanzibar (ZPL).
New City iliyokuwa inahitaji kushinda mechi tatu ili kufikisha pointi 35, huku ikicheza mechi 27 imeipa nafasi Mwenge kutanua mbawa kwa kuchukua pointi tatu zinazomfanya ifikishe 32. Matokeo yameifanya New City kubakiwa na pointi 26 na mechi mbili mkononi ambapo hata ikishinda haziwezi kuwatoa katika janga la kuzifuata Inter Zanzibar na Tekeleza zilizotangulia Ligi Daraja la Kwanza.
Katika mchezo mwingine, Malindi imefikisha pointi 39 baada ya kuifunga Tekeleza ambayo tayari iimeshuka daraja mabao 2-0 katika Uwanja wa Finya Kisiwani Pemba.
Wakati New City ikipokea kilio hicho, Mlandege imepokea kicheko cha kuifunga Uhamiaji mabao 3-1, ikipanda kutoka nafasi ya nne hadi ya pili na kufikisha pointi 53.
Vita ya kuwania ubingwa Ligi Kuu imepamba moto kati ya Mlandege, Mwembe Makumbi, KVZ naMafunzo ingawaje kwa Mwembe Makumbi imepoteza ramani baada ya juzi kufungwa na Kipanga mabao 2-0 na kumfanya kushuka hadi nafasi nne.
Hivyo, itamuiwa vigumu kutoboa katika katika michezo mitatu aliyoishikilia mkononi ikiwemo Mafunzo, KVZn na Malindi kwani wote wanauhitaji ubingwa msimu huu.