Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kwa Namungo ni heshima na nafasi

NAMUNGO Pict

Muktasari:

  • Namungo ipo nafasi ya 10 katika msimamo wa ligi imecheza mechi 28 imeshinda nane, sare saba, imefungwa 13 imekusanya pointi 31, hivyo ikishinda dhidi ya Kagera Sugar na KenGold itafikisha alama 37 na itategemeana na matokeo ya timu zilizopo juu yake.

KIRAKA wa Namungo, Erasto Nyoni amesema mechi mbili zilizosalia kufunga hesabu za msimu huu, zimebeba heshima na nafasi endapo timu hiyo ikishinda zote, inaweza ikapanda hadi nafasi ya tano iliyopo Tabora United.

Namungo ipo nafasi ya 10 katika msimamo wa ligi imecheza mechi 28 imeshinda nane, sare saba, imefungwa 13 imekusanya pointi 31, hivyo ikishinda dhidi ya Kagera Sugar na KenGold itafikisha alama 37 na itategemeana na matokeo ya timu zilizopo juu yake.

Jambo ambalo Nyoni mwenye mabao manne na asisti tatu alisema: “Japo tunakutana na timu zilizoshuka daraja, haina maana zitakuwa mechi nyepesi, tunajipanga kuhakikisha tunapata matokeo ya ushindi. Tunahitaji kumaliza nafasi za juu zaidi, endapo tukifanikiwa kupata pointi sita tutakuwa na alama 37 ambazo  ipo nazo Tabora United iliyo na michezo mitatu mkononi na itategemeana na itakachovuna katika mechi zake.”

Nyoni alisema msimu huu ulikuwa mgumu na ushindani, uliobeba taswira ya msimu ujao wa 2025/26 utakuwa mgumu zaidi.

“Msimu ujao utakuwa mgumu zaidi, timu zitasajili na zitajipanga zaidi, ninachofurahishwa nacho na wachezaji kuonyesha viwango vyao, vitakavyobadilisha maisha yao kiuchumi,” alisema.