Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ndanda FC yamsajili Mrisho Ngasa kuiua Simba

Muktasari:

Uongozi wa Ndanda umewatambulisha wachezaji watatu ambao imewasajili kwenye dirisha dogo tayari kwa mchezo wa kesho Jumamosi dhidi ya Simba.

Mtwara. Kuelekea katika mchezo wa Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara kesho Jumamosi dhidi ya Simba SC, Ndanda FC ya mkoani Mtwara imetangaza usajili wa wachezaji watatu waliongezwa kikosini katika dirisha dogo.

Katika tarifa ambao imetolewa na Ofisa Habari wa Ndanda FC, Idrissa Bandari amewataja wachezaji hao ni kiungo Mrisho Ngasa aliyemalizana na Mbeya City, mshambuliaji Ame Ali aliyekuwa Kagera na kiungo Salum Telela ambao wote wamesaini mkataba wa miezi Sita

“Tumefanya maboresho ya kuongeza watu wachache katika kikosi ambao tumewasainisha mkataba wa miezi sita tumeona wanaweza kuja kuhudumia katika kikosi chetu,” amesema Bandali.