Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ndanda FC mpo hebu wasikieni Kitayosce wanachosema

Muktasari:

Ni mchezo wa kombe la FA utakaopigwa uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara kwa mara ya kwanza tangu imepanda daraja la pili Kitayosce inacheza na Ndanda.

Mwanza. Kocha mkuu wa Kitayosce FC, Boniface Kiwale amesema wamejipanga sawa kuhakikisha wanashinda dhidi ya  Ndanda FC katika mchezo wa hatua ya 16 bora ya Kombe la FA utakaopigwa leo jioni kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.

Kiwale alisema anajua wanakutana na timu ngumu, lakini kikosi chake kipo sawa wataingia kwa tahadhari kuhakikisha wanapata ushindi.

Kocha huyo alisema leo asubuhi wamefanya mazoezi ya mwisho kwa ajili ya mchezo huo wa ugenini.

 “Ni mchezo mgumu kwetu, lakini tuko fiti kuwakabili Ndanda tutaingia kwa tahadhari kubwa kwani tunacheza na timu ya Ligi Kuu hivyo tunahitaji kuwaheshimu,” alisema Kiwale.

Alisema msimu huu wa kombe hilo wamejiwekea malengo ya kufanya vizuri kwani ana kikosi bora ambacho kinaweza kupambana na timu yoyote watakayokutana nayo.

“Nina kikosi kipana ambacho kina kiwango bora hivyo sina wasiwasi na timu yoyote nitakayopangiwa nayo kwenye haya mashindano” alisema kocha huyo.