Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ndanda FC inavyomrejesha Nduda kwenye makali yake

Muktasari:

Simba ilivyomsajili Nduda msimu uliopita, alidaka mechi mbili tu za ligi kuu dhidi ya Kagera Sugar na Majimaji ya Songea ikihitimisha kushuka daraja.

Dar es Salaam.KIPA wa Ndanda FC, Said Mohamed 'Nduda' amesema angalau anamaliza msimu huu vizuri baada ya kupata nafasi ya kufanya kazi tofauti na alivyokuwa Simba.

Simba ilivyomsajili Nduda msimu uliopita, alidaka mechi mbili tu za ligi kuu dhidi ya Kagera Sugar na Majimaji ya Songea ikihitimisha kushuka daraja.

Kitendo cha Simba kumtema katika usajili wa dirisha dogo, Nduda anasema kumemsaidia kumpa nafasi ya kucheza ambako kutalinda kipaji chake "Hakuna kitu kibaya kama mchezaji kukosa nafasi ya kucheza.

"Ili uwe mshindani lazima ucheze mechi nyingi, nimeanza kuwa fiti zaidi kwani huku asilimia kubwa ya mechi tangu nijiunge nao nimecheza, kitu ambacho ni kizuri kwangu.

"Ni kweli kuna uzuri na changamoto kucheza kwenye klabu kongwe na nimezichezea zote kwa maana ya Simba na Yanga kwa nyakati tofauti hivyo nazijua vilivyo na ndio maana nasema kutua kwangu Ndanda FC kunanirejesha kwenye makali yangu"anasema.