Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Namungo, Buswita kuyajenga upya

BUSWITA Pict

Muktasari:

  • Chanzo cha ndani kutoka Namungo, kilisema bado wanahitaji kusalia na Buswita, hivyo wamefungua mazungumzo mapya, ingawa mchezaji huyo ana ofa zingine mezani.

IMEELEZWA baada ya kiungo Pius Buswita kumaliza mkataba na Namungo FC, ameanza mazungumzo mapya na klabu hiyo, huku zikitajwa Geita Gold na Coastal Union kumpa ofa za kuhitaji huduma yake msimu ujao.

Chanzo cha ndani kutoka Namungo, kilisema bado wanahitaji kusalia na Buswita, hivyo wamefungua mazungumzo mapya, ingawa mchezaji huyo ana ofa zingine mezani.

“Kuna wachezaji wengi ambao wamemaliza mikataba yao na tunahitaji kuwaongezea, ukiacha Buswita, kuna Hussein Kazi,” kilisema chanzo hicho na kuongeza;

“Tunataka msimu ujao tumalize nafasi za juu zaidi ya nafasi ya 10 tuliyomaliza nayo na pointi 34 msimu uliopita, ndiyo maana tunahitaji kuwa na wachezaji ambao wataisaidia timu kwa moyo wa kuipambania.”

Alipotafutwa Buswita kuthibitisha taarifa hizo, alisema: “Ni kweli nimemaliza mkataba, najipa muda kidogo wa kupumzika baada ya hapo naamini kila kitu kitakaa sawa.”

Ingawa msimu ulioisha wa 2025-2026 haukuwa mzuri katika takwimu za ufungaji kwa Buswita alipomaliza bila bao, msimu wa 2023-2024 alimaliza na mabao saba huku 2024-2025 akitupia matatu.