Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Buswita alivyoporwa mrembo na mchezaji mwenzake

Muktasari:

  • Nyuma ya Kamera linaendelea na kukufichulia usiyoyafahamu ya mastaa mbalimbali nchini wanapoamua kuyasema na kuyaweka hadharani ambayo wengi hawayafahamu.

UKIWAONA katika kazi zao huwezi kuamini maisha yao nje ya wanachokifanya. Lakini ni wazi kila binadamu awe maarufu au asiwe, kuna mambo anayapitia ambayo anaamini hayapaswi kuwekwa wazi. Yapo mengi na kuna mengine yanaumiza zaidi na inapofikia mtu akaamua kukuambia ujue ni kweli lilimuumiza.

Nyuma ya Kamera linaendelea na kukufichulia usiyoyafahamu ya mastaa mbalimbali nchini wanapoamua kuyasema na kuyaweka hadharani ambayo wengi hawayafahamu.

Ndiyo. Usiyoyajua yanayoendelea au yaliyowatokea mastaa ni hapa na leo tumemfikia nyota wa Namungo FC, Pius Charles Buswita ambaye anasimulia namna alivyoumizwa na kitendo cha aliyekuwa mpenzi wake kuolewa na mchezaji mwenzake.

Wakati anajiunga Yanga 2017/2018, jina lake lilikuwa juu, akapata mrembo aliyeamini anampenda hadi kufikia hatua ya kutambulishana kwa ndugu na mipango yao ilikuwa siku moja kuingia kanisani kufunga ndoa takatifu.

Ndani ya miaka mitatu aliyocheza Yanga anasimulia penzi lao lilikuwa zito, mrembo huyo alikuwa akimposti katika mitandao ya kijamii akiambatanisha na maneno ya kimahaba, yaliyomshawishi nyota huyo kujiachia kwake na kumuona yupo eneo salama.

Anasema kuna wakati mrembo huyo, alikuwa akimuonyesha jumbe za wanaume wanazomtumia DM katika mtandao wa kijamii wa Instagram, akiwemo huyo aliyemuoa, kitu kilichomfanya aamini na kumwona ni mwaminifu ndiyo maana hamfichi kitu.

"Baada ya kuondoka Yanga, nilikwenda Rwanda kuichezea Kiyovu Sports, lakini sikukaa muda mrefu, ila wakati nipo huko kupostiwa kukapungua na simu hazikuwa nyingi kama nilivyokuwa Yanga na nilikuwa nakuta 'missed call' hata 10 na ujumbe juu," anasema Buswita na kuongeza;

"Msimu wa 2020/21, nilipojiunga na Polisi Tanzania kugombana kulikuwa hakuishi, nikaanza kusikia skendo zake za hapa na pale, ila nilikuwa nakaza moyo na kuweka imani kwake, kuona labda umbali ndiyo chanzo.

"Kwenye mpira wa miguu, ikitokea mpenzi wako katembea na mchezaji lazima utajua, maana kila timu unakuwa na washikaji zako wanakuambia mbona shemu anatoka na jamaa vipi mmeachana, wakati naenda Polisi Tz huyo mchezaji akawa anakuja kusaini timu ya Dar es Salaam, ambako kulikuwa na neema ya pesa.

"Hizi timu za mikoani  inatokea wakati mwingine mnakaa miezi mitatu bila mshahara, mwanamke anaweza akakuomba pesa ukimwambia asubiri anashindwa kuvumilia na hiyo ikawa nafuu kwa mchezaji mwenzangu kutumia gia hiyo kumpata na kitu kilichokuwa kinanikera zaidi, wakati nipo Yanga nilikuwa napenda kunyoa kama kiduku nakusokota kidogo juu, huyo mshikaji naye akaanza kunyoa hivyo hivyo, ikanibidi niachane na mtindo huo wa nywele, mbaya zaidi watu wanatufananisha kimo, mwili ni kama tunataka kufanana usoni, nilikuwa nikipita sehemu wananiita jina lake."

Mtihani mwingine anasema mwanzoni walikuwa wakikutana kwenye mechi ilikuwa inamuwia vigumu na mshkaji alikuwa na hofu:

"Washikaji wakawa wanasema mshikaji ana hofu sana, nikawaambia awe na amani nimeachilia, wamedumu hadi sasa na wamejaaliwa kupata watoto wawili."

Anakiri kisa hicho, kilimfanya asiwe na haraka ya kuoa akiamini asilimia kubwa ya wanawake wana tamaa, ila kwa sasa ana mpenzi ambaye hajui mambo ya mpira wa miguu na hana mambo mengi.

"Niliapa sitakuja kuoa mwanamke anayeshabikia mipira, anajua ratiba ya kila timu, nimempata mwingine na penzi letu kwa sasa lina utulivu, anajua nyakati nzuri na ngumu ninazopitia, maisha yanaendelea," anasema.