Nabi awatanguliza Mayele, Makambo

Kocha wa Yanga ameshusha sapraizi kubwa akianza na mastraika wawili mbele kwa mara ya kwanza dhidi ya Simba.
Nabi amewaanzisha washambuliaji wote wa taifa moja la DR Congo akianza na Fiston Mayele na Heritier Makambo.
Mchezo huu wa Nusu Fainali ya Kombe la Azam Shirikisho Nabi ameendelea na ukuta uleule ukiwa na kipa Diara Djigui,beki wa kulia Djuma Shaban kushoto Kibwana Shomari wakati mabeki wa kati wakiwa nahodha Bakari Mwamnyeto na Dickson Job.
Kwenye kiungo Nabi ameanza na viungo wanne Khalid Aucho,Yannick Bangala,Feisal Salum na Salum Aboubakar 'Sure boy.
Yanga ambao watacheza mfumo wa 4-4-2 wamewatanguliza washambuliaji Mayele na Makambo katika kusaka mabao.
Kwenye benchi Yanga imewapa nafasi kipa Aboutwalib Mshery,mabeki Ibrahim Abdallah,Paul Godfrey viungo wakiwa Zawadi Mauya,Jesus Moloko,Deuse Kaseke na Farid Mussa Huku washambuliaji wakiwa Chrispin Ngushi, na Chico Ushindi.