Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nabi atoa maelekezo makali kwa mastaa Yanga

KOCHA wa Yanga, Nasreddine Nabi amekuwa mkali kwelikweli. Anasema baada ya mechi dhidi ya Simba hataki kuona mchezaji wake yeyote akiishi kama msimu umeshamalizika.

Nabi alisema malengo ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu bado hayajafikiwa na huenda baada ya kutoka suluhu na Simba wachezaji wakawa wameridhika kama ambavyo baadhi ya mashabiki walivyo.

Yanga kwenye ligi imebakiwa na michezo tisa kati ya hiyo inahitaji kushinda mitano ili kutangaza ubingwa msimu huu bila ya kuangalia matokeo ya timu nyingine yoyote.

Michezo tisa iliyobaki nayo Yanga inacheza dhidi ya Ruvu Shooting (leo mjini Kigoma), Tanzania Prisons, Dodoma Jiji, Mbeya Kwanza, Biashara United, Coastal Union, Polisi Tanzania, Mbeya City na Mtibwa Sugar.

Alisema hataki kuona mzaha wowote kwenye mazoezi pamoja na mechi zilizo mbele yao na anataka kila mmoja kuwa makini, kujitolea na kupambana zaidi ya hapo awali ili kufanikisha lengo lao.

“Lengo ni kutwaa ubingwa wa ligi, sitaki kuona mchezaji yeyote anacheza kwa kuridhika na kuondoa ule ubora wake aliokuwa nao kabla ya mchezo dhidi ya Simba,” alisema Nabi na kuongeza;

“Ambacho nahitaji kutoka kwa wachezaji ni kujitoa zaidi katika michezo iliyobaki ili kupata pointi ambazo hazitafikiwa na timu yoyote ili kutwaa ubingwa huu wa ligi.

“Tunahitaji kuweka rekodi nyingine kama kuchukua ubingwa kwa pointi na mabao mengi, kutokupoteza mchezo, kuruhusu kufungwa mabao machache na nyingine na hatutaweza hayo bila ya wachezaji kujitolea,” alisema.

Katika hatua nyingine Nabi alisema wana haki ya kufurahi kwani si jambo zuri kwa timu kubwa kama Yanga kuishi misimu minne bila ya kutwaa ubingwa wa ligi pamoja na mafanikio mengine.

Nabi alisema ili kuonyesha kikosi cha Yanga kilikuwa bora msimu huu wanahitaji kufikia mafanikio mengine ya kutwaa ubingwa wa Kombe la Shirikisho (ASFC), waliyopo hatua ya nusu fainali.

Alisema msimu huu wametwaa ubingwa wa Ngao ya Jamii na sasa wanatakiwa kufanya hivyo kwenye ligi na ASFC na hayo yote yatawezekana kwa wachezaji wake kujitolea kwa kupambana kwenye kila mchezo ndio maana hataki kuona hata mmoja anacheza kwa kuridhika.

“Bado kuna kazi kubwa mbele yetu ili kumaliza msimu kwenye mafanikio baada ya kufikia yale malengo tuliyokubaliana kabla ya mashindano mbalimbali kuanza,” alisema Nabi.

Yanga kwenye ASFC wametinga nusu fainali wanamsubiri mshindi wa robo fainali kati ya Simba na Pamba (haijapangiwa tarehe).