Nabi apangua kikosi, watano warejea kikosini

Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi amepangua kikosi chake kitakachoivaa Geita Gold leo kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Katika kikosi kitakachoanza leo Nabi atawakosa wachezaji muhimu wa kikosi cha kwanza kilichopata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Kagera Sugar ambao ni Khalid Aucho, Saidoo Ntibazonkiza, Shaban Djuma na Farid Mussa ambao wanasumbuliwa na majeraha.
Nafasi zao zimezibwa na Dickson Job, Paulo Godfrey, Feisal Slaum, Yasin Mustapha na Deus Kaseke.
Ambapo wachezaji hao wote watano walikosekana katika mchezo uliopita lakini leo wamerejea kikosi cha kwanza kuikabili Geita Gold.
Katika mchezo wa leo Nabi ameanza na kipa Djigui Diarra, Paul Godfrey, Yasin Mustapha, Dickson Job, Bakari Mwamnyeto, Yanick Bangala, Denis Nkane, Abubakari Salum 'Sureboy', Fiston Mayele, Feisal Salum (Feitoto) na Deus Kaseke.
Wachezaji wa akiba ni Abuutwalib Mshery, Kibwana Shomari, Ibrahim Bacca, Zawadi Mauya, Mapinduzi Balama, Yusuph Athuman, Heritier Makambo na Dickson Ambundo.