Nabi abadili kikosi kuwavaa Mwadui

Sunday June 20 2021
KIKOSI PIC
By Ramadhan Elias

KOCHA mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amefanya mabadiliko katika kikosi chake cha kwanza kinachoingia uwanjani kucheza mechi ya Ligi Kuu dhidi ya Mwadui saa 1:00 usiku.

Katika mchezo huo utakaopigwa kwenye Dimba la Benjamin Mkapa, Nabi amefanya mabadiliko matatu katikakikosi chake tofauti na kile kilichoanza kwenye mchezo dhidi ya Ruvu Shooting Alhamisi ya juma lilopita na kshinda 3-2.

Eneo la kwanza alilofanyia mabadiliko ni kwa Kipa ambapp amemuanzisha Farouk Shikhalo kuchukua nafasi ya Metacha Mnata aliyesimamishwa kwa makosa ya kinidhamu.

Pia Nabi, amempanga Paulo Godfrey kucheza beki ya kushoto eneo ambalo katika mchezo na Ruvu, alicheza Adeyum Salehe.

Said Ntibanzonkiza ni mchezaji mwingine anayeanza leo katika kikosi cha Yanga ambaye mechi iliyopita aliingia akitokea benchi na nafasi yake alianza Farid Mussa ambaye leo kaanzia benchi.

Wachezaji wengine wanaoanza leo ni Kibwana Shomari, Dickson Job, Bakari Mwamnyeto, Tunombe Mukoko, Zawadi Mauya, Feisal Salum, Fiston AbdulRazack na Deus Kaseke.

Advertisement

Yanga inayowania ubingwa, inajitupa uwanjani kucheza na Mwadui inayokamilisha ratiba kwani tayari ilishashuka daraja hata kabla ligi haijamalizika.

Advertisement