Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mwinyi amlia mingo Oscar

 Haji Mwinyi

Muktasari:

Mwinyi aliyekuwa anasumbuliwa na majeraha ya nyama za paja katika mguu wa kulia, aliumia kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi, Zanzibar, alisema tayari ameanza kufanya mazoezi mepesi na Jumanne ya wiki ijayo atajiunga na kikosi chake.


BAADA ya kukaa nje takriban mwezi mmoja beki wa Yanga, Haji Mwinyi amesema anarejea kikosini akijiandaa na ushindani mkali wa namba dhidi ya  Oscar Joshua ambaye ameonyesha kiwango cha juu.

Mwinyi aliyekuwa anasumbuliwa na majeraha ya nyama za paja katika mguu wa kulia, aliumia kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi, Zanzibar, alisema tayari ameanza kufanya mazoezi mepesi na Jumanne ya wiki ijayo atajiunga na kikosi chake.

“Kutakuwa na ushindani mkali kwa sababu Oscar Joshua ni mzoefu na atakuwa ameitumia nafasi hiyo vizuri, lakini hilo litanisaidia kujituma zaidi kwa lengo la kufika mbali na si kuridhika kwa mafanikio niliyo nayo kwa sasa,” alisema.

Mwinyi alisema anaamini atarejea kwenye hali yake ya kawaida na kuendelea kuisadia klabu yake kwenye mbio za ubingwa ambao unaonekana kuwa mgumu msimu huu kutokana na uwepo wa michuano ya FA.

“Ligi Kuu msimu huu si lelemama kwa sababu nafasi ni finyu, lakini hilo pia litasaidia klabu itakayotwaa ubingwa kuonekana bora na yenye kiwango cha hali ya juu,” alisema.