Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mwenyekiti wa Kitayosce, kocha hatiani kwa upangaji matokeo

Muktasari:

  • Kitayosce FC iliyopo nafasi ya pili na pointi 57, kesho wanakutana na Afrikan Sport inayoshika nafasi 12 na pointi 23 kumalizia raundi 28 itakayoamua wao kupanda Ligi Kuu Bara kuifuata JKT Tanzania.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limewafungia maisha wanafamilia wawili wanaojishughulisha na mpira wa miguu, mwenyekiti wa Kitayosce Fc Yusuph Kitumbo na Kocha Ulimboka Mwakingwe kwa kosa la upangaji matokeo.

"Wawili haowalijihusisha na upangaji matokeo katika mechi ya Ligi ya Championship kati ya Fountain Gate FCna Kitayosce iliyochezwa Aprili 29 mwaka huu mjini Gairo, Morogoro" taarifa imesema

"Kamati ya maadili katika kikao chake kilichofanyioka Mei 11 mwaka huu imewatia hatiani kwa kuzingatia ibara ya 73(9)(b)ya kanuni za Maadili za TFF, Toleo la 2021".

Kitayosce FC iliyopo nafasi ya pili na pointi 57, kesho wanakutana na Afrikan Sport inayoshika nafasi 12 na pointi 23 kumalizia raundi 28 itakayoamua wao kupanda Ligi Kuu Bara kuifuata JKT Tanzania.