Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mwenge yaizima Junguni, Mwembe Makumbi ikibanwa ZPL

MWEMBE Piict
MWEMBE Piict

Muktasari:

  • Mwembe Makumbi iliyocheza mechi 24 ikivuna pointi 46, ikifuatiwa na Mlandege na Mafunzo zenye pointi 44 kila moja zikicheza mechi 23.

Maafande wa Zimamoto wameiwekea ngumu Mwembe Makumbi kwa kutoka sare ya 3-3, huku Mwenge ikiizima Junguni United katika mfululizo wa mechi za  Ligi Kuu Zanzibar.

Mwembe Makumbi ambao ndio vinara wa ZPL ilibanwa kwenye Uwanja wa Mao A, mjini Unguja.

Matokeo hayo yameifanya timu iliyopanda daraja msimu huu, ikifikisha pointi 46 kupitia mechi 24, ikiwa mbili zaidi na ilizonazo Mlandege na Mafunzo zenye 44 kila moja ikicheza mechi 23.

Rashid Said aliitanguliza  Zimamoto dakika ya tatu ya tu ya mechi hiyo kabla ya Mukrim Ali kuongeza chuma cha pili dakika ya 90 kwa penalti na kuizindua Mwembe Makumbi iliyofunga bao la kwanza dakika ya 22 kupitia Karim Salum.

Bao ni kama liliitia hasira Zimamoto kwani iliongeza bao la tatu dakika mbili kabla ya mapumziko kupitia Haruna Abdallah.

Kipindi cha Mwembe Makumbi ilirudi kivingine na kutengeneza mashambulizi makali yaliyoisaidia kurudisha mabao mawili katika dakika 10 za mwisho.

Mudrik Muhibu alifunga bao la pili kwa Zimamoto dakika ya 80 kabla ya Salum Omary kuchokomoa la tatu dakika ya 90+8 na kuikoa timu kupata kipigo.

Katika mechi nyingine iliyopigwa kwenye Uwanja wa Mao B,  Kipanga imekunjua makucha kwa kuiparua Malindi kwa mabao 2-1.

Mabao ya washindi yaliwekwa kimiani na Paul Matereza dakika ya 21 kwa penalti na Fredrick Godwin dakika ya 34 na Malindi ilipata la kufutia machozi dakika ya 87 likiwekwa kimiani na Said Omary.

Kwa upande wa Pemba,  Mwenge iliifyatua  Junguni United kwa bao 1-0  lililowekwa wavuni na Almas Himid dakika ya 42, katika pambano kali lililopigwa kwenye Uwanja wa FFU Finya.

Ligi hiyo itaendelea kesho kwa mechi tatu, KVZ itavaana na  Mlandege kwenye Uwanja wa Mao A, huku Tekeleza iliyoshuka daraja rasmi itaumana na Chipukizi Uwanja wa Finya na New City itakutana na Inter Zanzibar ambayo nayo imeshakata tiketi ya kucheza Ligi Daraja la Kwanza msimu ujao kwenye Uwanja wa Mao B.