VIDEO: Mwamnyeto, Nchimbi waipaisha Yanga, Saido azua gumzo

LIVE: Alichokifanya 'Saido Ntibazonkiza' leo | Nugaz amtaja Mwambusi

USHINDI wa mabao 3-1 waliopata Yanga dhidi ya Gwambina ni kama karibu kwa kocha wao mpya Nasreddin Nabi ambaye amesaini mkataba wa mwaka mmoja na nusu wa kukinoa kikosi hiko.

Mabao ya Yanga yalifungwa na Ditram Nchimbi, Bakari Mwamnyeto na Saido Ntibazonkiza huku bao la Gwambina likifungwa na Jimson Mwanuke.

Katika kipindi cha kwanza Yanga waliweza  kutawala mchezo na kwenda mapumziko wakiwa wanaongoza kisha katika kipindi cha pili  Gwambina walisawazisha dakika 49.

Katika kipindi  cha pili dakika 59 Ditram Nchimbi alikosa bao la wazi baada ya Kisinda kupiga krosi na Yacouba alipiga pasi ya kichwa kwa Nchimbi ambaye alikosa utulivu na kufyatuka shuti na kupita juu ya goli.

Yanga ilifanya mabadiliko dakika 66 kwa kumtoa Tusila Kisinda na kuingia Daido Nyibazonkiza, mabadiliko hayo yalitokana baada  ya Kisinda kuumia na kushindwa kuendelea na mchezo.

Mabadiliko hayo yalionekana kuwa na tija katika eneo la ushambuliaji katika kupeleka mashambulizi langoni kwa Gwambina.

Mwambusi alifanya mabadiliko mengine dakika 67 kwa kumtoa Yacouba Sogne na kuingia Michael Sarpong kwenda kuongeza nguvu.

Sarpong alionyesha utulivu wa kukaa na mpira kitu ambacho kilikosekana katika kipindi cha kwanza alipokuwa anacheza Yacouba Sogne.

Dakika 79 Gwambina walipata faulo nje kidogo ya lango la Yanga, Baraka Mtui alipiga faulo hiyo kwa ufundi lakini kipa Faruk Shikhalo aliydaka mpira huo.

Gwambina walifanya mabadiliko eneo la kiungo dakika 83 wakimtoa Yusuph Lenge na kuingia Salim Sheshe, wakati huo Gustapha Saimon alionyeshewa kadi baada ha kumfanyia madhambi Kaseke.

Dakika 85 Yusuph Kagoma alionyeshewa kadi ya njano baada ya kumfanyia madhambi Kibwana Shomari kwa kumnyooshea mguu juu.

Dakika 94 Saido Ntibazonkiza aligongeana pasi za haraka na Michael Sarpong kisha alionyesha utulivu baada ya kumtoka beki wa Gwambina na kufyatuka shuti lililokwenda moja kwa moja wavuni.

Baada ya bao hilo Ntibazonkiza alionyesha kutaka kutoka kwa kufanyiwa mabadiliko lakini hapo hapo mpira ulimalizika.