Mvua yaleta wasiwasi mechi ya Singida FG na Yanga

Muktasari:

  • Mvua hiyo imeanza saa 8:00 mchana na inaendelea kumiminika huku ikileta ugumu kwa mashabiki ambao wamejitokeza kukata tiketi, kuleta usumbufu wa kuingia uwanjani huku ikizua maswali kama baada ya mvua hiyo Uwanja wa CCM Kirumba utakuwa rafiki kwa mchezo huo kuchezeka.

Zikiwa zimebaki saa chache kabla ya kuanza kwa mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Singida Fountain Gate na Yanga utakaoanza saa 10:00 jioni, mvua kubwa inaendelea kunyesha katika jijini la Mwanza na kuleta hofu ya uwezekano wa mchezo huo kuchezwa kama kawaida.

Mvua hiyo imeanza saa 8:00 mchana na inaendelea kumiminika huku ikileta ugumu kwa mashabiki ambao wamejitokeza kukata tiketi, kuleta usumbufu wa kuingia uwanjani huku ikizua maswali kama baada ya mvua hiyo Uwanja wa CCM Kirumba utakuwa rafiki kwa mchezo huo kuchezeka.

Mmoja wa mashabiki ameliambia Mwanaspoti mvua hiyo imeharibu ladha ya mchezo huo ambao ulitazamiwa kuwa wa kuvutia.

"Mechi imeshaharibika hapa mvua yenyewe inaonekana haikati sasa hivi, usishangae tukaambiwa mechi imehairishwa hapa na sidhani kama uwanja utafaa tena," amesema shabiki huyo.