Mvua yaanza kujaza maji Uwanja wa Mkapa

Mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam zimeanza kujaza maji baadhi ya eneo la kuchezea la Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Mvua hizo ambazo zimeanza kunyesha mchana leo zimezalisha maji ambayo yameanza kuonekana yakijaa baadhi ya maeneo ya uwanja huo.

Hali hiyo inaleta wasiwasi juu ya hali itakavyokuwa baadaye wakati mchezo wa Hatua ya Makundi wa Kombe la Shirikisho Afrika kati ya wenyeji Yanga dhidi ya US Monastir utachezwa kuanzia saa 1:00 usiku