Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mukoko ndio basi tena Yanga

Mukoko ndio basi tena Yanga

Muktasari:

  • Klabu ya Yanga imethibitisha kiungo wake, Mukoko Tonombe kujiunga na TP Mazembe ya DR Congo kwa mkataba wa miaka miwili.

Dar es Salaam. Nahodha msaidizi wa Yanga, Mukoko Tonombe ameondoka rasmi ndani ya viunga hivyo baada ya kusaini miaka miwili TP Mazembe.

Kiungo huyo ametua kwa matajiri hao wa Congo baada ya kuhusishwa nao kwa muda mrefu na hatimaye yametimia.

Hapo awali ilisemekana dili la kiungo huyo kwenda Mazembe lilikufa baada ya kugoma kutolewa kwa mkopo katika klabu hiyo na kutaka kuuzwa.

Mabosi wa Yanga tayari walikuwa washakubaliana na mchezaji huyo kwenda Mazembe baada ya kuona hapati nafasi katika kikosi cha kwanza cha Nasreddine Nabi na pia kupata nafasi ya kumleta winga, Chico Ushindi ambaye alitua klabuni hapo akitokea TP Mazembe.

Katika dili la Yanga kumtaka Chico walitaka kumpeleka Mukoko kwa mkopo ili kumpata winga huyo.