Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chico: Tunabeba, mastaa Yanga wawekewa Sh70 milioni

WINGA mpya wa Yanga, Chico Ushindi ameangalia kikosi hicho akatamka; “Tunabeba.”

Staa huyo aliyesajiliwa dirisha dogo akitokea TP Mazembe ya DR Congo, leo jioni atacheza mechi yake ya kwanza Jijini Arusha timu yake itakacheza mechi ya kujifurahisha dhidi ya Mbuni FC.

Chico ameliambia Mwanaspoti kwa jinsi alivyoona ushindani kwenye mechi dhidi ya Coastal Union na hali ilivyo kambini na mazoezini ana uhakika Yanga itafanya vizuri msimu huu na ni aina ya timu zenye ushindani anaotaka yeye.

Alisema kwa timu alizoona kwenye vyanzo mbalimbali mpaka sasa anadhani Yanga ina nafasi kubwa ya kufanya vizuri kwa vile wana wachezaji wenye uwezo na hamu ya mafanikio.

“Ushindani ni mkubwa sana, sioni jinsi tunaweza kukosa ubingwa msimu huu. Sijaona timu zote lakini kwa ninachokijua mpaka sasa naona nafasi yetu ni kubwa,” aliongeza mchezaji huyo aliyekiri anatagemea ushindani mkubwa wa namba ndani ya kikosi.


USHINDANI

Chico anakuwa ni winga wa saba ndani ya kikosi cha Nabi, akipambana na Deus Kaseke, Dickson Ambundo, Denis Nkane, Jesus Moloko, Farid Mussa, Said Ntibazonkiza na Yacouba Sogne.

Kwenye idadi hiyo ya mawinga Nabi amekuwa akiwatumia mara kwa mara Moloko, Ntibazonkiza na Farid, hivyo ujio wa winga huyo kutoka Mazembe unatoa nafasi ya mchezaji mmoja kupungua kikosini.

Yacouba yupo nje ya uwanja kwa muda sasa kutokana na kusumbuliwa na jeraha la goti na nafasi yake Nabi amekuwa akimpanga Ntibazonkiza ambaye ameonekana kuwa vizuri akifunga mabao manne hadi sasa katika Ligi Kuu na kutoa pasi za mabao kwa wenzake.

Ntibazonkiza amekuwa tegemeo Yanga kwa mapigo ya mipira iliyokufa, akifunga bao kwa frii-kiki ya moja kwa moja na penalti, huku pia akipiga kona na adhabu ndogo zote na kutokana na uwezo wake wa kuchezesha timu na kutengeneza nafasi za kufunga, ni wazi nyota huyo wa Burundi ana uhakika wa namba kikosini.

Farid, hajafunga bao lakini amehusika katika mabao kadhaa muhimu ya Yanga msimu huu, likiwamo la ushindi wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba lililofungwa na Fiston Mayele Septemba 25, 2021 kwenye Uwanja wa Mkapa na la juzi alilomtengea Saido na kuwapa kujiamini Yanga wakishinda 2-0 dhidi ya Coastal Union kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga. Kwa ushindi huo Yanga walipewa Sh70 milioni.

Jesus Moloko amehusika moja kwa moja katika mabao nane kwenye michuano yote, akifunga mabao manne, ametoa asisti mbili na kusababisha penalti mbili, hivyo ni kati ya watu muhimu zaidi katika ushambuliaji wa Yanga huku akiwa mchapakazi anayesaidia sana ulinzi kwani hushuka mara kwa mara wanaposhambuliwa.

Yanga imemsajili staa wa Biashara United, Nkane ambaye alikuwa na mabao mawili katika timu yake ya zamani na ametua kwa kishindo Yanga akifunga bao moja katika Kombe la Mapinduzi.

Ujio wa ushindi unaweza kuwatikisa zaidi Ambundo, ambaye amerejea kutokea kuwa majeruhi na Kaseke ambaye msimu uliopita alitengeneza pacha ya kutisha na Yacouba, lakini msimu huu amekosa nafasi ya kucheza mara mara.

Akizungumza na Mwanaspoti, Ushindi alisema amekuja Yanga baada ya kuzungumza na Kocha Nabi Mohamed ambaye alimweleza anachotaka aje kufanya ambacho ni kuongeza kasi ya upatikanaji wa mabao.

“Naweza kufunga na kutengeneza mabao kwa wengine, naamini tukishirikiana mambo yatakuwa rahisi,” alisema Ushindi.


WADAU WAFUNGUKA

Winga wa zamani wa Yanga, Edibily Lunyamila amesema usajili ni mapendekezo ya kocha hivyo kuja kwa Ushindi huenda Nabi kuna kitu kakiona ndani yake ambacho hakuna mchezaji mwingine anacho.

“Yanga imekosa mataji mara nne mfululizo inatengeneza kikosi cha ushindani, inahitaji wachezaji zaidi ya wawili ndani ya eneo moja ili akikosekana mmoja kusiwe na pengo linaloweza kuwaathiri,” alisema na kuongeza;

“Ukiangalia Yanga ya sasa injini yao kubwa ni Khalid Aucho alivyoumia uliona namna ilivyotetereka, hivyo kuja kwa huyo winga siwezi kumzungumzia moja kwa moja sababu sijamwona akicheza, tumpe muda tutaona alichokiona Nabi kwake hadi akamleta katika eneo ambalo tayari lina wachezaji,” alisema.

Kiungo wa zamani wa Simba na Yanga, Athuman Idd Chuji alisema ujio wa Ushindi usiwatishe wachezaji waliokuwepo cha msingi ni kila mmoja kupambana kuhakikisha anapata nafasi.

Alisema, wingi wa mawinga ndani ya Yanga inamfanya na kocha Nabi kuwa na uchaguzi sahihi wa amtakaye.