Mukoko, Farid warejea kuiua Namungo

Mukoko, Farid warejea kuiua Namungo

Lindi. Kukosekana kwa kiungo Khalid Aucho kumemfanya kocha wa Yanga Nasreddine Nabi kumuanzisha Mukoko Tonombe katika mchezo wa leo dhidi ya Namungo.
Mukoko alianza katika mechi moja tu dhidi ya Ruvu Shooting  kati ya mechi Tano ambazo Yanga imecheza hadi sasa.
Katika mchezo huo dhidi ya Ruvu Shooting, Mukoko alifunga bao na kisha kuangua kilio kwa furaha na leo amerejea tena kikosi cha kwanza baada ya Aucho kuwa nje ya Uwanja kutokana na majeraha aliyoyapata wakati akiitumia timu ya Taifa ya Uganda.
Ukiondoa hiyo ya Ruvu Shooting ambayo ndivyo pekee alianza kikosi cha kwanza, hakucheza kabisa katika mechi tatu dhidi ya Kagera Sugar, Geita Gold na KMC lakini alikaa benchi katika mechi dhidi ya Azam.
Pia katika kikosi hicho Leo Nabi amemuanzisha kikosi Cha kwanza winga Farid Mussa kuchukua nafasi ya Yacouba Sogne aliye majeruhi.
Farid alianza katika mechi moja tu dhidi ya Kagera Sugar waliyopata ushindi wa bao 1-0 lakini akapigwa benchi mechi nyingine zote ziliofuata dhidi ya Geita Gold, KMC, Ruvu Shooting na Azam.
Kikosi Cha Yanga Leo ni Djigui Diarra, Kibwana Shomari, Djuma Shaban, Bakari Mwamnyeto, Dickson Job, Mukoko Tonombe, Jesus Moloko,Yannick Bangala, Fiston Mayele, Feisal Salum na Farid Mussa.