Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mukoko atakata Yanga ikiiua Mbuni

MABAO mawili ya penalti kutoka kwa kiungo Mukoko Tonombe dakika ya 55 na 81 ndio yaliiwezesha Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mbuni FC katika mchezo wa kirafiki uliopigwa kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

Mukoko alifunga bao la kwanza baada ya mshambualiaji Crispin Ngushi kumnawisha mchezaji wa Mbuni FC, Pascal Mwakapusya katika eneo la hatari huku bao la pili akifunga baada ya winga Chico Ushindi kufanyiwa madhambi katika eneo la hatari.

Katika mchezo huo kocha Nasreddine Nabi na msaidizi wake Cedrick Kaze waliamua kuwatumia wachezaji wengi ambao wamekuwa hawapati nafasi ya kuanza katika kikosi cha kwanza ambapo golini alisimama Erick Johola akisadiwa na Paul Godfrey, David Brayson ambaye aliumia dakika ya 38 na nafasi yake kuchukuliwa na Crispin Ngushi.

Wengine ni, Mukoko Tonombe, Ibrahim Abdullla, Zawadi Mauya, Dickson Ambundo, Salum Abubakar, Heriter Makambo, Farid Mussa na Deus Kaseke ambaye alimpisha Chico Ushindi katika dakika ya 64 huku nyota Fiston Mayele, Feisal Salum, Yanick Bangala, Abutwalib Mshery, Bakari Nondo, Denis Nkane Saido Ntibazonkiza, Yassin Musatapha, Yusuph Athuman na Jesus Moloko wakiwatazama wenzao jukwaani.

Kitu ambacho kilikuwa kinawavutia mashabiki wengi wa soka Arusha ni jinsi Mukoko Tonombe alivyokuwa akicheza kama mlinzi wa kati namba nne kwa umakini zaidi na kuwapata ugumu washambuliaji wa Mbuni FC kupenya ngome ya Yanga akisaidiana na Ibrahim Abdulla kwani wengi wamezoea kumuona akicheza kama kiungo namba sita.

Kocha Msaidizi wa Yanga, Cedric Kaze alisema wameamua kuwatumia wachezaji wengi ambao hawakupata nafasi katika mchezo uliopita dhidi ya Coastal Union yote ikiwa ni katika kuwapa nafasi wachezaji wote lakini pia ikiwa ni maandalizi kuelekea mchezo dhidi ya Polisi Tanzania FC.

"Mchezo ulikuwa mzuri japo kipindi cha kwanza hatukucheza vizuri sana pia kukosa nafasi nyingi za wazi lakini vijana wamepambana tumeibuka na ushindi kikubwa tulitaka wapate mazoezi," alisema Kaze.

Alisema kwa sasa wanaenda kuwandaa wachezaji vyema kwani mchezo wa Jumapili dhidi ya Polisi ambao utapigwa uwanja wa Ushirika wanataka kushinda hili kuendelea kuwa juu kwenye msimamo lakini pia kuongeza gepu la pointi dhidi ya timu ambazo ni wapinzani wao katika kuwania ubingwa.

Kocha wa Mbuni FC, Leonard Budeba alisema walitumia mchezo huo kama maandalizi kuelekea katika mechi za First league zilizosalia pamoja na mashindano ya kombe la shirikisho la Azam (ASFC), huku akiahidi kufanyia marekebisho sehemu ambazo ameona kuwa na mapungufu kabla ya kuanza kwa ligi.