Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mudathir aibeba Azam FC ikichapa Polisi Tanzania, Ndanda, Biashara United, Namungo zagawa dozi

Kipa wa Azam, Razak Abarola akidaka penalti iliyopigwa na Sixtus Sabilo wa Polisi Tanzania katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.PICHA NA MICHAEL MATEMANGA

Muktasari:

Matokeo hayo Azam FC imefikisha pointi 44 itaendelea kukaa nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara hata kama Yanga baadae itashinda dhidi ya Mbeya City haitaweza kuzifikia pointi za Azam FC.

Dar es Salaam. Bao la kiungo Mudathir Yahya ameifungia Azam bao pekee wakichapa Polisi Tanzania kwa 1-0 kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Mudathir alifunga bao hilo pekee kwa shuti kali katika dakika 48, lililomshinda kipa wa Polisi Tanzania, Mohamed Ally na kujaa wavuni.

Matokeo hayo Azam FC imefikisha pointi 44 itaendelea kukaa nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara hata kama Yanga baadae itashinda dhidi ya Mbeya City haitaweza kuzifikia pointi za Azam FC.

Polisi Tanzania watajilaumu wenyewe kwa kupoteza mchezo huo baada ya kupata penalti katika kipindi cha kwanza lakini mshambuliaji wake Sixtus Sabilo alikosa wakati timu yake ikilazimisha suluhu na Azam katika dakika 45 za kwanza.

Polisi ilipata nafasi ya kupata bao hilo baada ya Sabilo kupiga krosi iliyomgonga mkononi beki wa Azam, Daniel Amoah katika eneo la penalti.

Mwamuzi wa mchezo huo Thabiti Manika kutoka Ruvuma akaamuru penalti ipigwe kuelekea lango la Azam FC ambapo Sabilo kapiga shuti lililoangukia mikononi mwa kipa Razak Abalora.

Licha ya timu hizo kushambuliana kwa zamu ndani ya dakika 20 mpira haukuwa na kasi huku wachezaji wa Polisi Tanzania wakionekana wamechoka zaidi.

Polisi Tanzania nje ya penalti waliyoipata dakika ya nane, safu yake yake ya ushambuliaji ilishindwa kutumia nafasi zilizokuwa zinatengenezwa na viungo wao.

Dakika ya 28, Sabilo alipata nafasi nyingine ndani ya 18 ambapo shuti lake likapanguliwa na beki wa Azam FC, Yakub Mohamed na kuwa kona iliyodakwa na Abalora.

Mshambuliaji wa Azam FC, Obrey Chirwa alijikuta anashindwa kufurukuta mbele ya mabeki wa Polisi Tanzania ambao hawakumpa nafasi ya kuchezea mipira ndani ya 18 yao.

Katika michezo mingine, Biashara United ikiwa nyumbani ilipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mbao FC shukrani kwa bao la Atupele Green katika dakika 63.

Ndanda imeendeleza rekodi yake ya ushindi baada ya kuichapa Mwadui Fc kwa mabao 2-0 kwenye uwanja wa Mwadui Complex, Shinyanga.

Katika mchezo huo mabao ya Ndanda yalifungwa na Samwel John katika dakika 69, na Ommary Khamis (89).

Kagera Sugar ikiwa nyumbani Kaitaba ilikubali kipigo cha bao 2-1 kutoka kwa Alliance, Safari ya Singida United kushuka daraja imezidi kushika kasi baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Namungo kwenye Uwanja wa Namfua, Singida.

Lipuli ikiwa nyumbani imelazimishwa sare 1-1 na JKT Tanzania.

MECHI IMEAHIRISHWA

Mchezo kati ya Ruvu Shooting dhidi ya Tanzania Prisons uliokuwa uchezwe kwenye Uwanja wa Mabatini mkoani Pwani umeahirishwa baada ya gari ya huduma ya kwanza (Ambulance) kuchelewa kufika uwanjani hapo.

Kikosi

Azam FC: Razak Abalora, Nico Wadada, Bruce Kangwa, Yakubu Mohamed, Agrey Moris, Daniel Amoah, Abdallah Masoud, Salum Abubakar, Obrey Chirwa, Mudathir Yahya na Richard Djodi.

Akiba: Mwadini Ali, Abdul Omary, Salim Hoza, Idd Seleman, Idd Kipagwile, Never Tiger na Donald Ngoma.

Polisi Tanzania: Mohamed Ally,Shaban Stambuli, Yassin Mustafa, Mohamed Kassim, Iddy Mobby, Henrico Kayombo, Sixtus Sabilo, Jimmy Shoji, Erick Msagati, Anton Matheo, Athanas Mdamu.

Akiba: Peter Peter, Juma Haji, William Karote, Mohamed Mmanga, Pius Buswita, Simon Daniel na Mohammed Mkopi.