Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mtibwa yasaka kocha, yamkomalia Bayser

MTIBWA Pict

Muktasari:

  • Mtibwa iliyokuwa katika Ligi Kuu tangu 1996 ilishuka msimu uliopita baada ya miaka zaidi ya 25, lakini imekomaa Ligi ya Championship msimu huu na kuwa mabingwa ikipanda daraja sambamba na Mbeya City, huku timu ya tatu inasubiri mshindi wa jumla wa play-off ya ligi hiyo na yule wa Ligi Kuu.

MTIBWA Sugar kwa sasa inafanya mambo mawili muhimu, ipo katika mchakato wa kumtafuta kocha mkuu ndani na nje na kupitia kwa uongozi wa serikali Mkoa wa Morogoro inamshawishi, Jamal Byser kurudi kikosini.

Taarifa za ndani zinasema baada ya mabosi wa klabu hiyo kufanya kikao na kupitia ripoti ya mwenendo wa timu hiyo, umegundua aliyekuwa mwenyekiti wa zamani, Bayser amehusika katika mafanikio makubwa ikichukua ubingwa 1999 na 2000 na pengo lake halijazibika licha ya kuja viongozi wapya.

“Kuna viongozi wa serikali Morogoro wamekuwa wakizungumza na Bayser ili awe mhimili mkubwa wa timu irejee katika ushindani wa nafasi za juu na siyo kujikwamua kushuka daraja kama ilivyofanyika takribani miaka minne mfululizo,” kilisema chanzo hicho na kuongeza.

“Benchi la ufundi ambalo limepandisha timu halitavunjwa, Ligi Kuu inahitaji kocha mkuu awe na Leseni A na Awadh Juma ‘Maniche’ ana leseni B hivyo atakuwa msaidizi, jambo hilo linafanywa kwa haraka ili apatikane awe sehemu ya usajili wa nyota watakaoitumikia timu msimu ujao.”

Msemaji wa klabu hiyo, Thobias Kifaru alipotafutwa ili kuthibitisha taarifa hizo alisema: “Kuhusu kumtafuta kocha ni kweli, jambo lingine ndani ya wiki mbili atapatikana mtu wa kukabidhiwa usimamizi wa ujenzi wa majukwaa na viti vya kukalia mashabiki.”

“Kabla ya kuanza kwa msimu  kila kitu kitakuwa tayari na mashabiki wataangalia mechi wakiwa wamekaa na siyo kusimama, kuhusu Byser sifahamu chochote,” aliongeza Kifaru.

Mtibwa iliyokuwa katika Ligi Kuu tangu 1996 ilishuka msimu uliopita baada ya miaka zaidi ya 25, lakini imekomaa Ligi ya Championship msimu huu na kuwa mabingwa ikipanda daraja sambamba na Mbeya City, huku timu ya tatu inasubiri mshindi wa jumla wa play-off ya ligi hiyo na yule wa Ligi Kuu.