Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mtibwa yarudi mzigoni na mzuka mwingi

Muktasari:

  • Tangu walipomaliza mechi ya wanandugu Mtibwa Sugar dhidi ya Kagera Sugar waliyotoa sare ya bila mabao Machi 12, wachezaji walipewa mapumziko ya wiki moja na tayari wamerudi kambini.

BAADA ya mapumziko ya siku saba, Mtibwa Sugar imerejea tena mzigoni huku kocha mkuu wa timu hiyo, Zuberi Katwila akiahidi kukisuka vyema kikosi chake ili kujinasua mkiani.

Tangu walipomaliza mechi ya wanandugu Mtibwa Sugar dhidi ya Kagera Sugar waliyotoa sare ya bila mabao Machi 12, wachezaji walipewa mapumziko ya wiki moja na tayari wamerudi kambini.

Timu hiyo kongwe nchini haijawa na matokeo mazuri licha ya kufanya mabadiliko kwenye benchi la ufundi ambapo hadi sasa wapo mkiani kwa pointi 16 baada ya michezo 20.

Mtibwa Sugar ilianza msimu na Habibu Kondo ambaye baadaye alitemwa baada ya mabosi kutoridhishwa na matokeo na kumkabidhi mikoba Katwila ambaye alitokea Ihefu.

Katwila alisema kwa muda waliotoa mapumziko kwa mastaa, anaamini kila mmoja amebadilika kisaikolojia hivyo wanapoanza mazoezi ataisuka upya timu hiyo na kung’atuka mkiani.

“Tunajua ligi ni ngumu kwa sababu tumeachana pointi chache, hatuna matokeo mazuri ila lolote linawezekana benchi la ufundi tunaendelea kutengeneza upya muunganiko na kusahihisha makosa ya jumla,” alisema Katwila.

Nahodha wa timu hiyo, Oscar Masai alisema wanaporudi kambini watakuwa makini kusikiliza na kutekeleza maelekezo ya kocha wao kuhakikisha ligi inaporudi wanafanya kweli.

“Tusichopenda ni kuona timu inashuka daraja na tutahakikisha mechi 10 zilizobaki tunafia uwanjani kutafuta pointi tatu-tatu, sisi wachezaji tuko imara na tayari kuipambania Mtibwa,” alisema nyota huyo.