Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mtibwa yachapwa, mashabiki wawaka

MBEYA KWANZA imeonyesha ubabe mbele ya wakongwe kwenye Ligi Kuu Bara, Mtibwa Sugar kwa kuchukua pointi tatu, Uwanja wa Mabatini,  Pwani nje ya jiji la Dar es Salaam.


DAKIKA 20 ZA KWANZA
Licha ya Mbeya Kwanza, kucheza Ligi Kuu Bara kwa mara ya kwanza, ukuta wao ulicheza kwa nidhamu na walikuwa makini kukumbushana majukumu yao.

Mabeki ambao walifanya kazi kubwa ya kuwadhibiti washambuliaji wa Mtibwa Sugar ni Mizaa Christom (beki 2), Joseph Majagi(beki 5), Godfrey Muha(beki 4) na  Salum Chuku (beki 3).

Kiungo wa Mtibwa Sugar, Said Ndemla pamoja na kucheza kwa kiwango kikubwa,mabeki hao walicheza kwa nidhamu ya kumdhibiti.

Ukiachana na ukuta wao kuwa imara, safu yao ya mbele ilionekana kuwasumbua mabeki wa  Mtibwa Sugar, ikiongizwa na Hamis Kanduru na Paul Peter aliyekuwa anacheza nyuma ya straika  Christian Ngushi.

Hata hivyo mabeki wa Mtibwa Sugar, Ibrahim Ame, Geofrey Kiggi, Issa Rashid 'Baba Ubaya na Hassan Kibailo walitumia  uzoefu wao Kuwadhibiti washambuliaji wa Mbeya Kwanza.


BAADA YA DAKIKA 29

Dakika ya 29 straika wa Mtibwa,  Salum  Kihimbwa alikosa bao la wazi,alifanikiwa kupenya ngome ya Mbeya Kwanza na kubakia na kipa Hamad Juma,akapiga pasi ya mkaa.

Mtibwa Sugar ilionekana kubebwa zaidi na uzoefu wa kuzuia kasi ya wachezaji wa Mbeya Kwanza, huku Ndemla alipambana kuweka uhai eneo la kiungo.
Dakika ya 42 kipa wa Mbeya Kwanza, alitaka kufanya makosa ya kutaka kumpiga kanzu Kelvin Sabato 'Kiduku' mabeki wake wakawahi kusawazisha makosa.

Dakika 43 Kihimbwa alifika ndani 18 na kuchelewa kufanya maamuzi ya kuupiga mpira ambao ungeweza kuzaa matunda na badala yake kuweka krosi hafifu na kumkuta Kelvin Sabato aliyepiga shuti lililoishia mikononi mwa golikipa wa Mbeya Kwanza.


KIPINDI CHA PILI KILIVYOKUWA

Mbeya Kwanza, ilirejea kwa kasi kipindi cha pili ambapo dakika ya 49 straika wao, William Edgar alifunga bao la kuongoza kwa shuti kali nje ya 18.

Baada ya Edgar  kufunga bao hilo, alijikuta akilia kwa furaha kwa kufunga bao lake la kwanza.


Dakika ya 62 kocha Awadhi alifanya mabadiliko ya kuwaingiza  Kibaya, Riphat/ waliotoka ni Awadhi na Makang'a

Dakika ya 62 Khamis Kanduru wa Mbeya Kwanza, alipewa kadi ya njano kwa kosa la kumchezea rafu na Juma Ganambali.

Dakika  74 Mtibwa Sugar walifanya mabadiliko ya kumtoa Ndemla na walimuingiza Makarani.

Sabu nyingine waliofanya Mtibwa Sugar, dakika 83 kocha alimtoa Kihimbwa nafasi yake ilichukuliwa na ZIlimtusa Boban, wakati Mbeya Kwanza iliwatoa Kanduru na Ngushi, waliochukua nafasi zao ni Oscar Matanga na Chesko Mwasimba.


KELELE ZA MASHABIKI WA MTIBWA SUGAR
Baada ya washambuliaji wao, kushindwa kutumia nafasi za kufunga walizopata mashabiki walisikika walisema wamechoka kucheza mtoano.

"Tumechoka kucheza mtoano, kauli mbiu yetu ni ubingwa, jitumeni jamani," walisikika wakisema kwa uchungu mashabiki hao.