Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Msolla: GSM amebeba mzigo mkubwa

Muktasari:

GSM wamerejesha furaha kwa wanachama wa Yanga tangu alipoondoka aliyekuwa mwenyekiti wa klabu hiyo, Yusuph Manji.

MWENYEKITI wa klabu ya Yanga, Dk Mshindo Msolla amesema ufadhili wa kampuni ya GSM umekuwa kama mzigo kwao kwani wanajitolea kwa sehemu kubwa.

Msolla amesema kampuni hiyo imekuwa ikijitoa na kufanya nje ya sehemu ya makubaliano ya mkataba wao.

Msolla amesema GSM toka mwaka juzi kwenye dirisha dogo wamekuwa wakisimamia usajili kwa asilimia 100.

"GSM wamekuwa wakijitoa kwa kiasi kikubwa, usajili wote toka mwaka juzi wao ndio wanafanya mpaka sasa na ndio maana mnaona tunasajili," alisema Msolla.

Msolla amesema hata upande wa kambi ya timu ya wakubwa wamekuwa wakijitoa kwa ukubwa wa asilimia 100.

"Sisi Yanga tunachofanya ni kulipa mishahara tu mpaka sasa huku gharama zingine zikiwa upande wa GSM," alisema Msolla.