Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mshery mtegoni kuivaa Mtibwa leo

Abutwalib Mshery

KIPA namba mbili wa Yanga, Abutwalib Mshery atakuwa langoni kukabiliana na waajili wake wa zamani Mtibwa Sugar kwenye mchezo wa mwisho wa Ligi.

Mtibwa Sugar wenye pointi 31 ipo ugenini dhidi ya Yanga, kwenye Uwanja wa Mkapa ikisaka pointi tatu muhimu kwaajili ya kujiakikishia nafasi ya kubaki Ligi Kuu Bara msimu ujao.

Kikosi cha Yanga ni Mshery, David Bryson, Kibwana Shomari, Bakari Mwamnyeto na
Ibrahim Abdallah 'Bacca' eneo la ulinzi huku nafasi ya kiungo ikichezwa na Feisal Salum.

Nyota wengine kwenye kikosi cha Yanga ambao ndio mabigwa wa msimu huu ni Deus Kaseke, Jesus Moloko, Dickson Ambundo na Farid Mussa.

Kocha Nasreddine Nabi ameanza na mshambuliaji Fiston Mayele ambaye ndiye kibara wa upachikaji wa mabao kwenye kikosi hicho.

Hadi sasa kipa huyo amecheza michezo 19 kwenye Ligi Kuu Bara kati ya hizo 11 alikuwa Mtibwa Sugar na nane Yanga ameweka rekodi ya nyavu zake kutokutikiswa mara 10 kati ya michezo hiyo.

Mshery atakuwa na wakati mgumu kuipambania timu yake isivunje rekodi ya kutokufungwa huku akiwa na mtihani wa kuisaidia timu yake ya zamani kutokushuka daraja.

Mtibwa ipo nafasi ya 12 baada ya kucheza mechi 19 na kufanikiwa kukusanya pointi 31 huku wapinzani wao Yanga wakiwa nafasi ya kwanza kwa kukusanya pointi 71.