Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mrithi wa Mayele atambulishwa Yanga

Muktasari:

  • Mrithi huyo wa Mayele msimu uliopita katika ligi ya Ghana alifanikiwa kufunga mabao 15 kwenye mechi 26 na kutoa assist 3 akimaliza nafasi ya pili.

Klabu ya Yanga imefanikiwa kuinasa saini ya mshambuliaji, Hafiz Konkoni (23) Bechem United ya Ghana kwa kandarasi ya miaka miwili.

Konkoni ambaye amesajiliwa kuziba pengo la Mkongomani Fiston Mayele anayetajwa kujiunga na Pyramid ya Misri baada ya msimu uliopita kumaliza na mafanikio ya kuwa mfungaji bora Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho Afrika.

Mrithi huyo wa Mayele msimu uliopita katika ligi ya Ghana alifanikiwa kufunga mabao 15 kwenye mechi 26 na kutoa assist 3 akimaliza nafasi ya pili.

Kabla ya Konkoni kusajiliwa na  Yanga alikuwa akihusishwa  klabu ya Al Hilal ya Sudan.