Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mrithi wa Kim bado kidogo tu

Muktasari:

  • Mkurugenzi wa ufundi TFF, Oscar Mirambo alisema kigezo kikubwa wanachotumia ni kumpata kocha wenye uzoefu mkubwa na soka la Afrika atakayetoa kilio cha Watanzania wengi waliokata tamaa na timu yao.

SHIRIKISHO la Soka nchini (TFF) limeanza mchakato wa kutafuta kocha mpya wa timu ya taifa, Taifa Stars wa kuchukua nafasio iliyoachwa wazi na Kim Poulsen aliyeondelewa na Mzambia Honour Janza kuishikilia kwa muda kabla ya kurudi nchini kwao kwa majukumu mengine.

Mkurugenzi wa ufundi TFF, Oscar Mirambo alisema kigezo kikubwa wanachotumia ni kumpata kocha wenye uzoefu mkubwa na soka la Afrika atakayetoa kilio cha Watanzania wengi waliokata tamaa na timu yao.

"Tunatambua tuna jukumu hapo Machi na kocha wa muda, Janza amepata nafasi nyingine Zambia hivyo mashabiki wetu watambue muda sio mrefu kuanzia sasa tutamtangaza," alisema Oscar aliyefichua hakuna mzawa aliyeomba nafasi hiyo hadi sasa katika maombi yaliyopo mezani mwao.

Stars inajiandaa na michezo ya kufuzu Fainali za Afrika (Afcon 2023) ikiwa kundi F na timu za Algeria, Niger na Uganda, ratiba ikionyesha itacheza na Uganda Machi 20 kisha kurudiana Uwanja wa Benjamin Mkapa Machi 27.

Baada ya hapo itacheza na Niger kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Juni 12 kisha kusafiri kucheza na Algeria Septemba 4.
Timu mbili za kila kundi ndizo zitakazofuzu fainali hizo zitakazofanyika nchini Ivory Coastal kati ya Januari 7 hadi Februari 4 mwakani.