Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mourinho apewa mwaka Yanga Princess

Muktasari:

  • Sasa habari za uhakika ni kwamba baada ya mazungumzo ya muda mrefu hatimaye Mourinho amekubaliana na viongozi wa timu hiyo kuinoa kwa msimu ujao.

MWANZONI mwa mwezi huu tuliripoti, ishu ya Kocha Mkuu wa Yanga Princess, Mzambia Charles Haalubono anatarajiwa kutimka kikosini hapo na kumpisha Edna Lema ‘Mourinho’.

Sasa habari za uhakika ni kwamba baada ya mazungumzo ya muda mrefu hatimaye Mourinho amekubaliana na viongozi wa timu hiyo kuinoa kwa msimu ujao.

Mmoja wa viongozi wa Yanga (jina tunalo) aliliambia Mwanaspoti kuwa, Edna tayari amesaini mkataba wa mwaka mmoja.

“Tunasubiri Kocha Charles amalizie kusimamia michezo miwili iliyosalia kisha tutamtangaza Edna kuwa kocha mkuu alitoa masharti ya kutaka majukumu ya kuingia sokoni mwenyewe kusajili ili kupata wachezaji wenye ushindani,” alisema kiongozi huyo.

Tulipomtafuta mwenyewe juu ya usajili huo aliendelea kusisitiza kuwa “Ni kweli sina mkataba na Biashara lakini tusubiri kama ni kweli mtajua tu.”

Edna sio mgeni katika kikosi hicho kwani kabla ya kwenda Biashara United ya Mara iliyopo Chamspionship aliwahi kupita Yanga Princess.