Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Morrison: Simba ilistahili ubingwa

BM (1)

Muktasari:

  • Morrison ambaye kwa sasa anakipiga KenGold, klabu iliyoshuka daraja Ligi Kuu Bara, alisema pamoja na kwamba si mchezaji wa Simba kwa sasa, moyo wake ulikuwa nao kwa ajili ya heshima ya taifa.

NYOTA wa zamani wa Simba na Yanfa, Bernard Morrison, amefunguka baada ya Wekundu kushindwa kutwaa ubingwa wa Kombe la Shirikisho Afrika, licha ya juhudi kubwa ilizoonyesha dhidi ya RS Berkane ya Morocco.

Morrison ambaye kwa sasa anakipiga KenGold, klabu iliyoshuka daraja Ligi Kuu Bara, alisema pamoja na kwamba si mchezaji wa Simba kwa sasa, moyo wake ulikuwa nao kwa ajili ya heshima ya taifa.

"Nimeumia sana, pamoja na kwamba mimi sio mchezaji wa Simba kwa sasa. Lakini kwa kawaida watu wote Watanzania tulikuwa tunahitaji ubingwa. Si ndiyo? Lakini bahati mbaya imekwenda tofauti," alisema Morrison.

Morrison ambaye ni raia wa Ghana alisisitiza, Simba ilistahili kutwaa ubingwa huo kwa kiwango ilichoonyesha, lakini maamuzi ya refa yalikwamisha ndoto hiyo ya kihistoria kwa klabu na taifa kwa ujumla.

"Kwa heshima ya Tanzania, nadhani mwamuzi hajasaidia Simba. Sijafurahia, kuna vitu vingi hajafanya vizuri. Tunatakiwa kukubaliana na hilo. Awamu hii, kwa kweli Simba ilistahili kubeba ubingwa huu  lakini ndio mpira ulivyo, kuna kushinda na kuna kupoteza," alisema.

Akiwa Zanzibar kushuhudia fainali hiyo ya kihistoria, Morrison alisema alikwenda kama Mtanzania kushangilia timu ya nyumbani kwa lengo la kutoa sapoti si kwa Simba pekee, bali kwa Tanzania nzima.

"Mimi nimekuja huku kushangilia Simba, kushangilia Tanzania. Kwa sababu Simba ingebeba kombe, ni heshima kwa Tanzania. Watu wangesema ni Simba, lakini mwisho wa siku ni Tanzania iliyoshinda," alisema.

Morrison pia alieleza upendo wake kwa baadhi ya wachezaji wa Simba aliowahi kucheza nao, akitaja kwa heshima kubwa kama kina Shomari Kapombe, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ na kipa Aishi Manula.

"Wachezaji wote wa Simba nawapa heshima, lakini Kapombe, Tshabalala na Aishi hawa mara zote wamekuwa watu wangu. Aishi ni namba moja wa Tanzania. Hata kama atakaa nyumbani miaka 10, itabaki hivyo. Hakuna kipa Tanzania anayemkaribia Aishi. Hana wa kumfananisha naye," aliongeza Morrison.

Kauli hiyo ya Morrison imeonesha namna ambavyo fainali hiyo ya Kombe la Shirikisho CAF haikuwa tu mchezo wa kawaida kwa mashabiki wa Simba, bali ilikuwa suala la taifa matumaini na heshima ya Watanzania wote barani Afrika.

Simba ilitoka sare ya 1-1 dhidi ya RS Berkane kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar, matokeo ambayo hayakutosha kuwapa ubingwa baada ya kupoteza mchezo wa kwanza 2-0 nchini Morocco.