Moloko, Bryson kuikosa Mtibwa, Sure Boy arejea

KIKOSI cha Yanga kinaondoka leo Februari 21 tayari kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mtibwa Sugar Februari 23 Mwaka huu kwenye Uwanja wa Manungu Morogoro.
Mhamasishaji wa klabu hiyo, Haji Manara anasema timu inaondoka mchana wa leo huku ikitarajia kuwakosa baadhi ya mastaa wao wanaokabiriwa na majeraha.
Anasema kwenye mchezo huo wanatarajia kumkosa Jesus Moloko, Abdallah Shaibu na David Bryson huku akimtaja Aboubakal Salum ‘Sure Boy’ na Yassin Mustafa kurudi baada ya kukaa nje kwa muda.
“Maandalizi kwa upande wa timu yanakwenda vizuri na tunakwenda Manungu tukiachana na histori zilizopita tunafuata pointi tatu muhimu ili kuendeleza mpango kutwaa taji,”
“Mtibwa Sugar ilishawahi kuwa bingwa mara mbili mfululizo ni timu ya kuheshimiwa wanauzoefu mkubwa wana misimu 25 kwenye Ligi ukitoa Simba na Yanga hakuna timu iliyocheza mfululizo ligi bila kushuka,” anasema.