Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mlandege yajiweka pazuri mbio ubingwa ZPL

ZNZ Pict

Muktasari:

  • Timu tano zilizopo katika mbio za  ubingwa wa Ligi Kuu Zanzibar msimu huu ni: watetezi JKU, KVZ, Mafunzo, Mlandege na Mwembe Makumbi, huku nne zinazopambana kuepuka kuungana na Tekeleza na Inter Zanzibar katika kushuka daraja ni; Chipukizi,  Junguni United, Mwenge na Kipanga.

MABINGWA wa Kombe la Mapinduzi, Mlandege imeendelea kuufukuzia ubingwa wa Ligi Kuu Zanzibar (ZPL), baada ya kuichapa Mwenge kwa bao 1-0 katika mechi iliyopigwa jana kwenye  Uwanja wa Mao A, mjini Unguja.

Bao hilo pekee lililoipa Mlandege poinri tatu muhimu lilifungwa na Mussa Hassan dakika ya 63.

Licha ya Mlandege kutoka na ushindi, lakini  ilionekana haina muunganiko na wachezaji walikuwa wanapoteana wakati wakutengeneza nafasi za mashambulizi katika lango la Mwenge.

Matokeo hayo yameifanya Mlandege ambao ni mabingwa wa Kombe la Mapinduzi kwa msimu wa pili mfululizo imefikisha pointi 50 kupitia mechi 26.

Katika mechi nyingine, Watetezi wa Ligi hiyo, JKU ilitakata kwa kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Chipukizi kwenye Uwanja wa FFU Finya uliopo visiwani Pemba. 

Yakoub Amour ndiye aliyefunga bao hilo  dakika ya sita tu ya mchezo na kudumu hadi dakika 90.