Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mkude, Sureboy, Farid wakacha paredi la Yanga

Muktasari:

  • Jana Yanga ilitetea ubingwa wa nne wa Kombe la Shirikisho la FA ikiichapa Singida Black Stars mabao 2-0 na kufikisha makombe matano ambayo imeyatwaa msimu huu baada ya awali kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu Bara, Ngao ya Jamii, Kombe la Muungano pamoja na Kombe la Toyota.

Wakati wachezaji wa Yanga na benchi la ufundi la timu hiyo wakiingia kwenye gari tayari kwa ajili ya kuanza msafara wa Paredi la Yanga, mastaa watatu hawakuingia kwenye gari hilo.

Jana Yanga ilitetea ubingwa wa nne wa Kombe la Shirikisho la FA ikiichapa Singida Black Stars mabao 2-0 na kufikisha makombe matano ambayo imeyatwaa msimu huu baada ya awali kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu Bara, Ngao ya Jamii, Kombe la Muungano pamoja na Kombe la Toyota.

Wakati wachezaji wa Yanga wakiongozwa kuingia kwenye gari maalumu lililobeba wachezaji na benchi la ufundi ili kuanza paredi Mkude,'Sureboy na Farid Mussa walipita njia yao.

Licha ya muongoza msafara wa wachezaji kuwaelekeza njia ya kuingia lakini Mkude aliwaongoza wenzake wapite njia nyingine na wakaingia gari ya peke yao.

Ni nyota hao watatu ambao hawajaingia kwenye gari hilo lakini nahodha Bakari Mwamnyeto na msaidizi Dickson Job ndiyo walioongoza msafara huo ambao umeanzia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.