Mjipange, hili ndilo jeshi la Gwambina

Muktasari:
Baada ya kupanda Ligi Kuu ikiwa kinara wa Kundi B ilipomaliza ikiwa na pointi 47, hivi sasa wanalenga kumaliza nafasi za juu kufika fainali kwenye Kombe la Shirikisho
DIRISHA la usajili wa wachezaji wa soka lililofunguliwa Agosti Mosi na litafungwa mwishoni mwa mwezi.
Timu mbalimbali zikiwataja wachezaji waliosajiliwa na walioachwa. Gwambina FC ni moja ya timu itakayoonekana mara ya kwanza msimu ujao wa Ligi Kuu sambamba na Ihefu FC na Dodoma Jiji FC.
Gwambina FC imetaja wachezaji 25 wanaounda kikosi ikiwa ni pamoja na ingizo jipya na wengine waliokuwapo tangu Daraja la Kwanza (FDL).
Gwambina FC imefanikiwa kumnasa Kocha Mwinyi Zahera ambaye amekwenda kuwa mkurugenzi wa Ufundi.
INGIZO JIPYA
Wachezaji wapya wako 10 ambao ni pamoja na Stali Nyambe (Buildcon FC-Zambia) ambaye anacheza nafasi ya kipa.
Mabeki: Aaron Lulambo kutoka KMC FC, Lameck Daniel (Biashara United), Baraka Mtui “Popa” (Ruvu Shooting) na Novartus Lufunga (Lipuli FC).
Kiungo: Said Mkangu (Sahare All Stars)
Washambuliaji: Paul Nonga (Lipuli FC), Moric Mahela (Stand United), Japhet Makalai (Kagera sugar) na Miraji Saleh wa Stand United.
UONGOZI
Mwenyekiti wa timu hiyo, Omari Mmassy anasema wamefunga usajili na wachezaji wameanza mazoezi.
Anasema nafasi iliyobaki ya kusajili ni kwa ajili ya wachezaji wa U20 ambao kocha atawapandisha kutokana na viwango vyao.
“Lakini kama ataona anahitaji kusajili mchezaji yeyote bado tunaweza tukafanya hivyo maana muda unaturuhusu na nafasi bado zipo,” alisema Mmassy.
Uongozi wa timu hiyo unaendelea na maboresho ya uwanja wao katika mapungufu yaliyojitokeza kwenye michezo ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL).
Mmassy anasisitiza uwanja huo utakuwa tayari kwa michezo yote 36 ya ligi pamoja na mashindano ya FA hata katika michezo ya Simba, Yanga na Azam FC itapigwa kwenye uwanja huo uliopo wilayani Misungwi.
KIKOSI KAZI
Uongozi wa Gwambina FC juzi uliweka bayana sura ya timu hiyo kwa msimu wa mwaka 2020/21 hadi sasa kikiwa na jumla ya wachezaji 25 huku 10 ikiwa ingizo jipya. Hiki ndicho kikosi kamili cha Gwambina FC.
Mkurugenzi wa Ufundi:
Mwinyi Zahera
Kocha mkuu:
Novatus Fulgence
Makocha wasaidizi:
1. Athuman Bilal
2. Hassan Mwakami
Kocha wa viungo:
Seleman Kisendi
Kocha wa makipa:
Kibwana Nyogoli
Meneja wa timu:
Mrisho Gambo
Meneja vifaa:
Godfrey Daniel.
Daktari wa timu:
Elisha Cosmas.
WACHEZAJI
Makipa:
1. Mohamed Makaka-Ruvu shooting
2. Isihaka Ibrahim- Gwambina FC
3. Stali Nyambe- Buildcon FC, Zambia
4. Mohamed Hussein- Gwambina FC
Mabeki:
1. Revocatus Richard- Gwambina FC
2. Salum Kipaga- Gwambina FC
3. Hamad Nassor- Gwambina FC
4. Anthony Matogoro- Gwambina FC
5. Aron Lulambo- KMC FC
6. Lameck Daniel- Biashara United
7. Baraka Mtui “Popa”- Ruvu Shooting
8. Novartus Lufunga-Lipuli FC
Viungo
1. Yusuph Kagoma-Gwambina FC
2. Yusuph Lwenge ‘Dunia’-Gwambina FC
3. Salim Juma Sheshe-Gwambina FC
4. Rajab Athuman-Gwambina FC
5. Said Mkangu-Sahare FC
6. Jacob Massawe-Gwambina FC
Washambuliaji
1. Meshack Abraham-Gwambina FC
2. Jimmyson Steven-Gwambina FC
3. Paul Nonga-Lipuli FC
4. Kapama Kibadeni-Gwambina FC
5. Moric Mahela-Stand United
6. Japhet Makalai-Kagera Sugar
7. Miraji Saleh-Stand United