Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mgunda amtaka Okrah

KIWANGO bora alichoonyesha mshambuliaji wa Simba, Augustine Okrah kimeonekana kumvutia kocha Juma Mgunda aliyeeleza ubora wake umetokana na mbinu mbalimbali alizokuwa anampatia.
Mgunda alisema baada ya kupewa timu aliwapa hali ya kujiamini wachezaji wote na kila mmoja kuhisi yupo kwenye timu kwa ajili ya kutoa mchango wake ili iweze kufanya vizuri ndio maana walisajiliwa 30.
Alisema wakati anapewa majukumu ya kukinoa kikosi cha Simba Okrah alikuwa anacheza kiungo wa ushambuliaji ila alimbadilisha na kumtumia winga wa kushoto kutokana na uwezo wake wa kutumia mguu wa kushoto.

"Mabidiliko hayo yalitokana na ubora alionyesha mazoezini kwani ni nafasi aliyokuwa akitumika vizuri tangu akiwa Ghana niliamini atakwenda kucheza kwenye ubora zaidi ya awali na kweli imekuwa hivyo kwa sasa," alisema Mgunda na kuongeza;
"Kwa kushirikiana na wachezaji wengine Okrah amekuwa katika kiwango bora ikiwemo kufunga kama ilivyokuwa mchezo dhidi ya Yanga, kutoa pasi za mwisho kama mechi dhidi ya Primiero de Agosto ugenini,"
"Naamini si Okrah tu bali wachezaji wote ndani ya Simba wamekuwa na mabadiliko tofauti na hapo awali kutokana na vile ambavyo naishi nao, majukumu niliyowapatia na mbinu mbalimbali ambazo nawaelekeza kwenye kiwanja cha mazoezi.
"Naendelea kutengeneza kikosi cha Simba imara kukosoa makosa ya mchezaji mmoja mmoja pamoja na yale ya timu kuboresha kiwango cha timu na wachezaji wote ili kufanya vizuri katika mashindano yote ya ndani pamoja na Ligi ya mabingwa Afrika."
Kwa upande wa Okrah alisema alisajiliwa na Simba kuhakikisha anatoa mchango kwa kuonyesha kiwango bora kila mechi ili aweze kuipa mafanikio timu ikiwemo kushinda michezo mingi.
Okrah alisema kila kocha huwa na mtazamo wake kulingana na mchezaji alivyo kuna namna wanaamini anaweza kucheza kwenye nafasi fulani ila kwake hilo halina shida kwani anaweza kucheza nafasi zote za mbele pamoja na beki wa kushoto.
"Naonekana kuwa na kiwango bora kutokana na kufuata yale maelekezo ya kiufundi ambayo napatiwa na kocha ila si rahisi kufanya hivyo mwenyewe bila ya ushirikiano kutoka kwa wachezaji wenzangu," alisema Okrah mwenye mabao mawili Ligi Kuu Bara na kuongeza;
"Nahitaji kuonyesha kiwango bora na kupambana zaidi ya wakati huu ili Simba ipate mafanikio tofauti na ilivyokuwa msimu uliopita kwani hilo ndio dhumuni kubwa kwa upande wetu na baada ya kukamilika hilo mafanikio mengine binafsi ya mchezaji huwa yanakuja tu."