Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mganda afichua siri ya Diarra

KIPA wa Biashara United, Mganda James Ssetuba amewachambua makipa wazawa na wageni akiwamo Diarra Djigui kwenye Ligi Kuu huku akitaja kinachowabeba wageni na kupewa nafasi zaidi mbele ya wazawa.

Ssetuba ni miongoni mwa makipa watatu wa kigeni wanaoanza kwenye vikosi vyao sawa na Diarra wa Yanga, Jonathan Nahimana wa Namungo na Mathias Kigonya wa Azam na hapa ameweka wazi sababu za wao kufanya vizuri.

“Nadhani mifumo ni tofauti, mfano mimi tangu mdogo nilikuwa kwenye akademi hivyo kila kitu nimefundishwa ngazi kwa ngazi.

Kingine ni kujiamini na kujifunza kila siku kutokana na makosa, mfano kipa kama Diarra unamuona anavyojiamini sawa na Kigonya au Nahimana, wote wanajiamini sana na hiyo inawasaidia wanapokuwa langoni,” alisema Ssetuba na kuongeza;

“Cha mwisho ni uzoefu kwani unakuta kipa hadi kufika Tanzania kafundishwa na makocha tofauti wenye ubora na mbinu tofauti hivyo hiyo pia inatusaidia kwani tuna mchanganiko wa makocha wengi.”

Tangu amejiunga na Biashara msimu uliopita Ssetuba amekuwa kipa namba moja na kumuweka nje Daniel Mgore ambaye pia ni bora katika eneo hilo.