Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Metacha: Vita ya clean sheet si mchezo

METACHA Pict

Muktasari:

  • Metacha ambaye katika mechi 19 alizocheza msimu huu  anamiliki clean sheet saba alisema akiondoa vinara Moussa Camara wa Simba mwenye clean sheet 15) na Djigui Diarra wa Yanga mwenye 14, amefurahishwa na ushindani wa makipa wazawa akiwamo Patrick Munthari wa Mashujaa mwenye 12.

KIPA wa Singida Black Stars, Metacha Mnata amesema Ligi Kuu Bara imezidi kunoga, kwani kumekuwa na vita ya makipa kuonyesha ubora, huku akiwamwagia sifa wenzake kwa kuchuana vikali.

Metacha ambaye katika mechi 19 alizocheza msimu huu  anamiliki clean sheet saba alisema akiondoa vinara Moussa Camara wa Simba mwenye clean sheet 15) na Djigui Diarra wa Yanga mwenye 14, amefurahishwa na ushindani wa makipa wazawa akiwamo Patrick Munthari wa Mashujaa mwenye 12.

Metacha alisema licha ya ubora wanaouonyesha Camara na Diarra, lakini makipa hao wamezungukwa na vitu vingi vya kuwabeba kufanya vizuri kama uzoefu na ubora wa mabeki walionao, tofauti na makipa wa timu nyingine.

"Ninapozungumzia uzoefu ni wa kucheza michuano ya kimataifa kupitia timu zao na timu za taifa mfano Ibrahim Bacca, Dickson Job kutoka Yanga, Simba kuna Mohamed Hussein 'Tshabalala' , Shomari Kapombe wa Simba hao wote wana uwezo mkubwa wa kuwasaidia makipa wao kufanya vizuri,  kwani wamecheza michuano mbalimbali ya kimataifa ambayo imewaaaidia viwango vyao kuwa bora, hivyo ninapoona kipa kama Munthari anastahili pongezi kwani anajitajidi kujitoa kadri awezavyo," alisema Metacha na kuongeza;

"Makipa wengine ambao wamekuwa na viwango vya juu msimu huu ni Yona Amosi wa Pamba (clean sheets 9), Suleiman Yakubui wa JKT Tanzania (clean sheets 8) hao wote ni wazawa ambao watakuwa na faida kwa timu ya taifa Stars, hivyo wanastahili kupewa mauwa yao ."

Pamoja na hilo alikiri uwepo wa Camara na Diarra, kumeongeza chachu ya ushindani na mvuto eneo la makipa.

"Siwezi kukwepa kukiri ubora wa makipa hao kama wazawa vipo vitu vingi vya kujifunza kutoka kwao, kama utulivu katika kufanya maamuzi ya kuokoa hatari za washambuliaji wa timu pinzani," alisema.

Mtazamo wa Metacha haujatofautiana na kipa Amos aliyesema: "Kwa upande wangu naona makipa wazawa tunapambana tuwezavyo kuonyesha viwango vyetu, ingawa wanaoongoza kwa clean sheets ni wageni."