Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Messi vs Ronaldo : Kwa wafuasi Ronaldo hakamatiki Facebook,Twitter

Muktasari:

Kwenye Instagram Ronaldo ana watu wanaomsoma milioni 33 akiwa amemzidi Neymar Jr. Ronaldo pia ni mwanamichezo maarufu zaidi kwenye Twitter akiwa anasomwa na watu wapatao milioni 43 na kwa ujumla anashika nafasi ya 14 akiwa nyuma ya mastaa wengine wa dunia kina Katy Pery, Justin Bieber na Taylor Swift na wengineo

KATIKA toleo ililopita, mwandishi, Luca Caioli alichambua ugomvi uliojitokeza kati ya Ronaldo na kocha wake wa Real Madrid, Rafa Benitez na jinsi ambavyo Ronaldo hakufurahia kitendo cha kocha huyo kumpa somo la upigaji mipira ya adhabu. Sasa endelea…

“Ananifundisha mimi kuhusu mipira ya adhabu lakini pia namna nzuri ya kushambulia na mpira na namna ya kupiga chenga.”

Ushauri wa aina hiyo Ronaldo hakukubaliana nao, ni matukio ambayo aliamua kuyageuza hatua ambayo mchezaji huyo angependa kuyasahau.

Kuna uwanja mmoja ambao hapana shaka kwamba Ronaldo ndiye bingwa mtawala, uwanja huo ni ule wa kwenye mitandao ya kijamii.

Kwenye eneo hilo Ronaldo hana wa kumsogelea ana watu wapatao 112 milioni wanaomsoma kwenye Facebook akiwa amemzidi mwanamuziki Shakira, hiyo ni hadi Machi 2015. Kabla ya hapo Shakira alikuwa kinara akiwa na watu 101 milioni wanaomsoma.

Kwenye Instagram Ronaldo ana watu wanaomsoma milioni 33 akiwa amemzidi Neymar Jr. Ronaldo pia ni mwanamichezo maarufu zaidi kwenye Twitter akiwa anasomwa na watu wapatao milioni 43 na kwa ujumla anashika nafasi ya 14 akiwa nyuma ya mastaa wengine wa dunia kina Katy Pery, Justin Bieber na Taylor Swift na wengineo.

Na umaarufu wake hauishii hapo, kwa mujibu wa ripoti ambazo zilichapishwa kwenye Hookit, Februari 23, 2016, Ronaldo alikuwa mwanamichezo wa kwanza kufikisha watu milioni 200 wanaomsoma kwenye Facebook, Twitter na Instagram, kuna wakati alikuwa akipata watu 135,000 kila siku.

Aliwahi kutoa shukrani zake kwenye Twitter aliposema, “Hakika ninajivunia kuwa mwanamichezo wa kwanza kuwa na watu milioni 200 wanaonisoma kwenye mitandao ya kijamii. Asanteni sana mashabiki wangu!” Salamu hizo za Ronaldo kwenye Twitter ziliandamana na ishara za kuonyesha furaha.

Mwingine aliyemfuatia akiwa na watu wanaomsoma milioni 78 alikuwa ni Messi, hata hivyo kilichoonekana ni kama haukuwa mlinganio sahihi kwa kuwa Messi hakuwa na akaunti ya Twitter. Na wa tatu alikuwa ni staa wa mpira wa kikapu wa NBA, Lebron James.

Ronaldo alijiunga na mtandao wa Twitter mwaka 2010 na tangu wakati huo ameposti matukio yapatayo 2,400 wastani wa matukio 40 kwa mwezi, mengi kati ya hayo yakiwa kwa lugha ya Kiingereza.

Kwenye mitandao ya kijamii Ronaldo ana watu wapatao milioni 100 anaowasoma (follows) amejizuia kutovuka kiwango cha mastaa wengine wa dunia kina Jennifer Lopez, Lady Gaga na Rafael Nadal pamoja na wanasoka kina Sergio Ramos na rafiki yake Fabio Coentrao.

Mvuto ambao Ronaldo anaupata katika mitandao ya kijamii ulimfanya ashawishike kuanzisha mtandao wake wa kijamii mwaka 2013 wa vivaronaldo.com, ambao ulikuwa huru kwa kila mtu ukiwa katika lugha ya Kiingereza.

Ni eneo ambalo mashabiki wake walipata fursa ya kubadilishana mawazo katika matukio mbalimbali yaliyojiri huku wakifuatilia mechi zote za Ronaldo na kuingizwa katika mashindano mbalimbali ambako washindi hupewa hure jezi zenye jina la Ronaldo au tiketi za kuangalia mechi anazocheza.

Pia hupata fursa ya kuangalia picha maalum na video za matukio mbalimbali, kumuunganisha Ronaldo na mashabiki na kujadiliana naye mambo mbalimbali.

Hata hivyo mtandao huo ulizimwa rasmi mwaka 2015, si kwa sababu haukuwa wenye mafanikio kwani hata timu iliyokuwa ikiusimamia iliahidi mambo makubwa kuwa njiani.

“Tumepata uzoefu ambao umetupa hamasa kuwapa fursa wafuasi wa kipekee wa Ronaldo kwa miaka miwili na nusu, mnaweza kuendelea kumuunga mkono Ronaldo kupitia Viva Ronaldo kwenye akaunti za Facebook, Twitter na Instagram.

“Asanteni kwa kuwa mashabiki bora duniani! Subirini ujio wa kilicho bora ambacho tunaendelea kukifanyia kazi, tunachokiandaa kitaendelea kuwapa myapendayo kuliko ilivyokuwa awali,’’ ilisema taarifa hiyo.

Itaendelea Jumamosi ijayo…