Mechi ya Simba vs Ndanda kukoleza safari ya ubingwa

Dar es Salaam. Safari ya Simba kuelekea kwenye hekaheka za ubingwa msimu wa 2017/18 imeelekezwa kwa Ndanda, ambapo mashabiki wa Simba wanaomba kila dua ili kuibuka na ushindi kwenye mchezo huo utakaopigwa mwishoni mwa wiki hii kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Hata hivyo, upande wa kikosi cha Ndanda hakuna mteremko kwa Simba kutokana na klabu hiyo kupigana kufa na kupona ili kuhakikisha inabaki Ligi Kuu.
Kibarua kigumu kwa Ndanda ni kuizuia timu hiyo yenye kiu ya ubingwa ambapo mwishoni mwa wiki iliyopita iliwatandika mabingwa watetezi wa Yanga baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0.
Ndanda ipo nafasi ya 15 kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 23 huku ikicheza jumla ya michezo 26.
Mechi ya Simba dhidi ya Ndanda FC kwenye Uwanja wa Taifa inatarajiwa kuwa na ushindani mkali kutokana na umuhimu wa mchezo huo kwa kila timu.