Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbrazili Simba afundisha kwa simu

Muktasari:

  • KOCHA Mkuu wa Simba, Roberto Oliveira 'Robertinho' atarejea nchini Januari 31, baada ya kukamilisha masuala yake ya kifamilia aliyokwenda kuyaweka sawa kwao Mbrazili, lakini akiwa huko ameendelea kuinoa timu kwa kutumia simu akiwatumia wasaidizi wake wanaoisimamia timu kwa sasa.

KOCHA Mkuu wa Simba, Roberto Oliveira 'Robertinho' atarejea nchini Januari 31, baada ya kukamilisha masuala yake ya kifamilia aliyokwenda kuyaweka sawa kwao Mbrazili, lakini akiwa huko ameendelea kuinoa timu kwa kutumia simu akiwatumia wasaidizi wake wanaoisimamia timu kwa sasa.

Robertinho aliyeiongoza Simba katika mechi mbili za Ligi Kuu Bara na zote kushinda dhidi ya Mbeya City na Dodoma Jiji, alitimka kwao wiki iliyopita na kuiacha timu chini ya wasaidizi wake, lakini akiwa huko ameliambia Mwanaspoti kila kinachoendelea kwenye mazoezi ya Simba haswa masuala ya kiufundi anayafahamu kwani kila kinachofanyika ni mpango wake akielekeza kwa simu.

Robertinho alisema kabla ya kuondoka nchini alifanya kikao kifupi na wasaidizi wake wawili, Juma Mgunda na Ouanane Sellami na kuwapatia programu na aina ya mazoezi yanayotakiwa kufanyika kwa kipindi cha wiki moja ambacho atakosekana.

Alisema tangu siku ya kwanza walipoanza mazoezi baada ya kumaliza jioni huwa nafanya mawasiliano nao kwa simu kwa kupata ripoti maalumu yenye kila kitu cha kiufundi kila zoezi kutoka na walichokuwa wanakusudia na yeye kuwapa maelekezo ya kipi cha kufanywa kwa simu inayofuata.

"Kikubwa maendeleo ni mazuri kwenye mazoezi yetu na kila kitu kimefanyika kama vile nilivyokuwa nahitaji kama kuna mapungufu yatakuwa ni machache na baada ya kurudi tutaunganisha nguvu kwa pamoja," alisema Robertinho na kuongezea;

"Jambo zuri lingine urejeo wa wachezaji wetu waliyokuwa majeruhi, tena wakiwa katika hali nzuri naamini hadi wiki ijayo wote watakuwa sawa na wataanza kucheza kama si mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Singida Big Stars basi ule wa Ligi ya mabingwa Afrika ugenini dhidi ya Horoya.