Prime
Mbrazili aitisha kikao na mastaa

Muktasari:
- Timu hiyo itarudiana na Dynamos Jumapili kwenye mechi ya raundi ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika, baada ya awali kutoka sare ya mabao 2-2 ugenini mjini Ndola, Zambia na sasa Wekundu hao wakihitaji ushindi wa aina yoyote au hata suluhu au sare isiyozidi bao moja kutinga makundi kwa mara nyingine.
SIMBA imeipiga Pan Africans mabao 4-0 ikiendelea kutengeneza hesabu za kuivaa Power Dynamos ya Zambia kwenye mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, lakini kocha wa timu hiyo, Roberto Oliveira ‘Robertinho’ akiitisha vikao tofauti na wachezaji ili kutengeneza mipango ya kutoka kwa Wazambia.
Timu hiyo itarudiana na Dynamos Jumapili kwenye mechi ya raundi ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika, baada ya awali kutoka sare ya mabao 2-2 ugenini mjini Ndola, Zambia na sasa Wekundu hao wakihitaji ushindi wa aina yoyote au hata suluhu au sare isiyozidi bao moja kutinga makundi kwa mara nyingine.
Sasa mara baada ya kuinyoa Pan Africans kwenye mchezo wa kirafiki uliopigwa juzi jioni, Robertinho amekuwa akiyajenga na mastaa wake akianza na wale wa ukuta.
Robertinho amekuwa akidili na mchezaji mmoja moja akianza na wale wanaocheza eneo hilo la ulinzi akiwapanga jinsi gani ya kucheza kwa utulivu kwenye mchezo huo.
Mbali na mabeki pia Robertinho amefanya vikao kama hivyo na wachezaji wanaocheza eneo la kiungo lakini pia wale wanaocheza mbele akijifungia na mchezaji mmoja mmoja.
Akizungumza na Mwanaspoti, Robertinho alisema nafasi kubwa imekuwa ni kuwatengeneza kisaikolojia wachezaji wa timu hiyo, huku akiwakumbusha pia juu ya ubora wa wapinzani hao waliotoka nao sare awali.
Robertinho alisema wanahitajika kucheza kwa nidhamu kubwa eneo la ulinzi ili kuhakikisha hawaruhusu mabao ambayo yatawatibulia hesabu zao lakini pia kuwa imara kwenye eneo la kiungo ambalo litatumika kutuliza ukuta wao na kutengeneza nafasi za mabao.
“Mabao mawili tuliyoyapata kule ugenini yatatusaidia hapa na wao yaliwaumiza lakini tunaporudi nyumbani hatutakiwi kuzubaa.”