Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbinu anazoweza kutumia mwanamichezo kupunguza unene

Muktasari:

Mtaalamu hutoa dawa hizo kwa watu ambao zao la uwiano wa uzito wa mwili na urefu wa mwili (body mass index) ni zaidi ya 30 au pengine ni 27 na huku tayari ameanza kupata madhara ya unene ikiwamo kuugua kisukari cha aina ya pili.

Ni jambo lisilopingika kuwa na unene/uzito uliopitiliza ni mojawapo ya matatizo ya afya yanayoikabili dunia kutokana na kuambatana na magonjwa sugu ikiwamo shinikizo la damu na kisukari.
Upunguzaji uzito wa mwili kwa kutumia dawa ni moja ya matibabu yanayowachanganya wananchi kutokana na kuwapo taarifa nyingi za mitandaoni kuhusu matabibu kuwa kuna dawa za kupunguza uzito wa mwili.
Kisayansi njia salama ya kukabiliana na unene ni mazoezi mepesi na ulaji sahihi wa vyakula kwa kuzingatia kanuni za afya.
Njia hii hasa kwa mazoezi ya kila siku ndiyo inakubalika kama nyenzo inayokabili unene ukilinganisha na dawa za kupunguza unene.
Katika huduma za afya hakuna dawa iliyoidhinishwa na ipo ndani ya miongozo ya matibabu ya kitaifa na kimataifa hasa ya Shirika la Afya Duniani (WHO) ambayo ni salama kupunguza uzito wa mwili.
Zaidi miongozo mingi inasisitiza unene uliokithiri au uzito mkubwa huweza kudhibitiwa kwa mazoezi na vyakula.
Bado taasisi nyingi za chakula na dawa duniani zinazitilia shaka usalama wa dawa za kupunguza uzito ndiyo maana hazipo katika miongozo ya matibabu.
Vipo vidonge ambavyo vimekuwa vikitumiwa mara kwa mara duniani katika nchi zilizoendelea ili kukabiliana na uzito wa mwili ambavyo ni Orlistat, Belviq, Contrave, Sexenda, Phentermine na Qsymia.
Baadhi ya dawa hizo zinafanyakazi za kuzuia unyonywaji wa mafuta na sukari mwilini katika mfumo wa chakula, nyingine huchochea homoni inayoutaarifu ubongo kuwa tumbo limejaa chakula na kukunyima hamu ya kula chakula.  Mtu anayeruhusiwa kuandika dawa za kupunguza uzito wa mwili ni daktari bingwa wa magonjwa ya ndani (physician) pekee,  kwa kuwa hizo dawa zina madhara makubwa ikiwamo kusababisha shambulizi la ghafla la moyo.
Mtaalamu hutoa dawa hizo kwa watu ambao zao la uwiano wa uzito wa mwili na urefu wa mwili (body mass index) ni zaidi ya 30 au pengine ni 27 na huku tayari ameanza kupata madhara ya unene ikiwamo kuugua kisukari cha aina ya pili.
Pia, inapoonekana mbinu ya vyakula na mazoezi mepesi imeshindikana, hupewa dawa.
Siyo kila mtu anaweza kutumia dawa hizo, ni lazima wataalamu wa afya wamfanyie uchunguzi mhusika kuona kama mwili wake utaweza kukabiliana na madhara yatakanayo na dawa hizo.
Mwandishi wa makala haya ni daktari wa binadamu.