Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbelwa, Mandonga kupeana vitasa Lindi

MANDONGA Pict

Muktasari:

  • Pambano la Light Heavy litachezwa siku ya Idd Pili na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

MABONDIA Karim Mandonga ‘Mtu Kazi’ na Said Mbelwa wanapeleka burudani ya ngumi mjini Ruangwa, Lindi.

Pambano la Light Heavy litachezwa siku ya Idd Pili na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Mapromota Tanzania, Everest Ernest alisema pambano hilo litaambatana na mapambano mengine 10 ya utangulizi yatakayojumuisha na mabondia kutoka Lindi.

Hilo litakuwa pambano la tatu kwa mabondia hao ambapo mawili yaliyopita moja Mandonga alishinda na la mwisho lilimalizika kwa sare.

Akijinadi kuhusu pambano hilo, Mandonga alisema amekuja na ngumi mpya aina ya Kaniki ambayo ndio ataitumia dhidi ya mpinzani wake.

Mbelwa alisema haamini kama Mandonga ni mtu kazi na hadi sasa bado hakubaliani na uamuzi wa pambano la mwisho walilokutana  ambalo lilimalizika kwa sare.