Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbaya wa Yanga nahodha Ndikumana afunga ndoa

Muktasari:

Ndikumana amesisitiza, anarudi Tanzania kwa ajili ya kuisaidia klabu yake ya Mbao katika mechi za Ligi Kuu pamoja na Kombe la Shirikisho.

BEKI na nahodha wa Mbao FC, Mrundi Yusuph Ndikumana ameamua kuuaga ukapera baada ya kufunga ndoa na  mchumba wake wa zamani, Zabibu Hassan.

Ndikumana amefunga ndoa na mchumba wake huyo ambaye pia ni Mrundi jana Alhamisi nchini kwao Burundi na baada ya hapo, ikafanyika sherehe fupi iliyohudhuriwa na mastaa mbalimbali wa soka pamoja na kocha wake wa Mbao, Mrundi Etienne Ndayiragije.

Baada ya kukamilisha shughuli hiyo, Ndikumana ameushukuru uongozi wa klabu ya Mbao FC, benchi la ufundi, wachezaji wenzake, mashabiki pamoja na wote waliofanikisha shughuli yake.

Na amesisitiza, anarudi Tanzania kwa ajili ya kuisaidia Mbao katika mechi zake za Ligi Kuu pamoja na Kombe la Shirikisho:

"Ni jambo la kheri kwangu kufunga ndoa na mke wangu Zabibu Hassan ambaye nampenda sana."

"Ni suala la kawaida kwangu kuipigania timu yangu ambayo ninaipenda sana ya Mbao, hivyo narudi nikiwa kamili,"anasema Ndikumana.

Nahodha huyo aliiongoza Mbao FC katika kuidhibiti Yanga mchezo wa wiki iliyopita ambao waliibuka na ushindi wa mabao 2-0.