Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mazembe: Yanga wanaenda robo fainali CAF

Muktasari:

  • Wakati Yanga ikilazimishwa sare ya bao 1-1 na wenyeji wao Real Bamako ya Mali mapema Mazembe walishtuliwa wakichapwa nyumbani kwa mabao 2-0 na vinara wa kundi lao US Monastir ya Tunisia.

MASHABIKI wa Yanga wanalia na timu yao kushindwa kupata pointi tatu za kwanza ugenini kwenye mechi za Hatua ya Makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika, lakini wapinzani wao TP Mazembe wameumia na sare hiyo zaidi kisha wakatoa tamko la nafasi yao.

Wakati Yanga ikilazimishwa sare ya bao 1-1 na wenyeji wao Real Bamako ya Mali mapema Mazembe walishtuliwa wakichapwa nyumbani kwa mabao 2-0 na vinara wa kundi lao US Monastir ya Tunisia.

Akizungumza na Mwanaspoti kwa njia ya simu akiwa jijini Lubumbashi nchini DR Congo, Kocha wa Mazembe Pamphil Mihayo alisema hatua ya Yanga kupata sare dhidi ya Real Bamako sio taarifa njema kwao hasa kuelekea mchezo wa marudiano.

Mihayo ambaye ni kiungo wa zamani wa Mazembe alisema taarifa pekee njema kwao sasa ni kusikia Yanga anapoteza huku nao wao wakiwa na mfupa mgumu wakitakiwa kushinda ugenini wakiwafuta Monastir.

Mihayo aliongeza kuwa hawawezi kukata tamaa na kwamba watashuka nchini Tunisia wakiwa na nguvu tofauti kushinda ugenini ingawa wanatambua kuwa haitakuwa rahisi.

“Tumejiweka katika mazingira magumu, kuna nidhamu tuliipoteza dhidi ya Monastir, kitu kibaya zaidi wenzetu Yanga nao wakatoa sare sio mbaya kwao kupata pointi moja lakini kwetu kama Mazembe hizo ni taarifa mbaya,” alisema Mihayo.

“Wakishinda (Yanga), nyumbani watakimbia zaidi lakini kitu kigumu tunatakiwa kukitafuta sasa ni kushinda kule Misri, utaona hizo ni hesabu ngumu lakini hakuna kinachoshindikana katika soka.

Aidha Mihayo ambaye alipoteza mchezo wa kwanza wa mashindano ya CAF tangu arejee kwenye timu hiyo, alisema Yanga bado anawaona wanaweza kuwa moja ya timu itakayofuzu kulingana na ratiba waliyobaki nay katika mechi tatu.

“Ukiangalia ratiba inawabeba Yanga kitu kikubwa ni kama watawafunga Bamako wakiwa nyumbani, pia kama wataambulia pointi moja au zote kwa Monastir, wakishindwa kuwafunga Bamako tunaweza kukimbizana nao hasa kama watapoteza na Monastir kwa kuwa sisi na wao tutakutana hapa kwetu hiyo itakuwa ni fainali ambayo Mungu atakuwa ametuletea.