Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mayele atambulishwa rasmi Pyramid

Pyramid FC ya Misri imemtambulisha rasmi mshambuliaji wa Kimataifa wa Congo DR Fiston Mayele kutokea Yanga

Alianza na mabao 16 msimu wa kwanza na kukikosa kiatu cha dhahabu kilichokwenda kwa George Mpole aliyekuwa Geita Gold na kufunga mabao 17 na katika msimu wa pili alitupia mipira 17 nyavuni na kumaliza kinara akilingana na Saido Ntibazonkiza wa Simba.

Msimu uliopita, alifunga mabao mengine 14 katika mashindano ya CAF. Alifunga kwanza mara saba katika mechi za awali za Ligi ya Mabingwa, kisha mengine saba katika Kombe la Shirikisho Afrika na Yanga ilifika fainali na kuzidiwa na USM Alger ya Algeria iliyotwaa ubingwa kwa faida ya bao la ugenini baada ya sare ya 2-2.
 
Mayele anaondoka Yanga baada ya kuisaidia kutwaa taji la Ligi Kuu mara 2, FA Cup 2 Ngao ya Jamii mara mbili na kuisaidia Yanga kucheza fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa mara ya kwanza katika historia yao msimu 2022/2023 na ndio Mfungaji bora wa Michuano hiyo akimaliza na magoli 7